PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Al-Shabab latangaza mauaji kupitia Facebook
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab ...



Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab
Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab

Kundi la wanamgambo wa Somalia Al-Shabab limesema limeuwa watu watatu ambao linawashutumu kwa kufanya upelelezi katika mashirika ya kijasusi ya Marekani au Somalia. Kundi hilo lenye uhusiano na al- Qaida lilitangaza mauaji hayo Jumanne katika ukurasa wake wa Facebook.
Wanaume hao watatu walipigwa risasi na kikosi cha walenga shabaha cha Al-Shabab katika mji wa Barawe


Limesema mmoja wa wanaume waliouawa mwenye umri wa miaka 29 Mohamed Abdulle Gelle aliongoza ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani kufanya shambulizi lililouwa kamanda wa Al- Shabab katika mji wa Juba nchini Somalia Oktoba mwaka jana.

Hilo likiashiria shambulizi lililomuuwa mtaalamu wa milipuko wa Al- Shabab aliyejulikana kama Anta, mwezi oktoba 28 mwaka jana.

Al-Shabab lilisema mtu wa pili, Ahmed Abudllahi Farole  mwenye umri wa miaka 47  alifanya  ujasusi kwa niaba ya serikali ya  jimbo la Puntland. Mwanamume wa tatu ambaye hakutambulishwa, alishtumiwa  kwa kufanya ujasusi kwa niaba ya serikali ya Somalia.

Taarifa hiyo ilisema wanaume hao watatu walipigwa risasi na kikosi cha walenga shabaha katika mji wa Barawe.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top