Al Shabaab
Wanamgambo wa kiislam nchini Somalia wameshambulia hoteli moja muhimu katika eneo la Kati mwa Somalia ambapo wanamgambo hao waliopoteza udhibiti wake wiki iliyopita .
Walioshuhudia shambulio hilo wameiambia BBC kuwa gari lililipuka nje ya hoteli katika mji wa Bulo-burde wanakoishi askari wa muungano wa Afrika na makamanda katika jeshi la Somalia .
Mlipuko huo ulifuatiwa na makabiliano ya risasi yaliyodumu kwa muda wa saa tano .
Walioshuhudia wanasema takriban watu kumi na wanne wameuawa katika shambulio hilo , ambalo wapiganaji wa al-Shabab wamesema walilitekeleza.
Mji wa Bulo-burde ulitwaliwa tena katika moja ya harakati za kijeshi zinazoendeshwa na vikosi vya Amison na vile vya serikali dhidi ya wanamgambo hao.
Post a Comment