HABARI ZA PWANI: Ajali yaua 21 Pwani, yajeruhi 10! A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: HABARI ZA PWANI: Ajali yaua 21 Pwani, yajeruhi 10! Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: WATU Ishirini na moja (21) wamefariki dunia na wengine 9 wamejeruhiwa vibaya, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa us... WATU Ishirini na moja (21) wamefariki dunia na wengine 9 wamejeruhiwa vibaya, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika kijiji cha Mkupoka, Wilayani Rufiji katika Mkoa wa Pwani. Ajali hiyo imetokea usiku wa jana Machi 30, mwaka huu, na kuhusisha gari la abiria aina ya Hiace T 948 CUX, lililokuwa likitokea Ikwiriri kwenda Jijini Dar es salaam, na lori aina ya Tata,T 132 AFJ lilokuwa limesimama barabarani ambapo katika harakati za kulipita ragi hilo aligongana na gari aina ya Mitsubishi T 774 CJW lililokuwa likielekea Ikwiriri. Habari zilizozithibitishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, amesema ajali hiyo imesababishwa na dereva wa gari la abiria, alipokuwa akijaribu kulipita lori,hilo ambalo lilikuwa likitokea Jijini Dar es salaam bila uangalifu. Kamanda Matei, amesema miili ya Marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Ikwiriri, na majeruhi wanaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Mchupwi. Hata hivyo amesema kwa sasa ndugu na Jamaa wanendelea kutambua miili ya marehemu, pamoja na majeruhi waliolazwa hospitalini na kuwataka Wananchi kuendelea kufika katika hospitali hiyo, kwa ajili ya kutambua miili ya watu wengine. Kwa Upande wake, MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, amesema baada ya ajali hiyo kutokea ilisababisha Vifo vya Watu 7 papo hapo, ambapo katika harakati za kuweka miili ya na majeruhi pembeni karibu na barabara, kulitokea basi la abiria kutoka Nachingwea na kukanyaga majeruhi wote na kuua waliokuwa wanaokoa, na kusababisha vifo vya Watu wengine 14, na kufanya idadi hiyo kuongezeka hadi kufikia 21.
Post a Comment