PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAWAKALA WA BIASHARA YA USAFIRISHAJI WATU WAKAMATWA JIJINI TANGA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Kamanda wa uhamiaji mkoa wa Tanga Kagimbo Bakar Na Mwandishi wetu Tanga maipacarusha20@gmail.com Jeshi la uhamiaji mkoa wa Tanga limefanik...

Kamanda wa uhamiaji mkoa wa Tanga Kagimbo Bakar



Na Mwandishi wetu Tanga

maipacarusha20@gmail.com


Jeshi la uhamiaji mkoa wa Tanga limefanikiwa kuwanasa Mawakala wanne wanaojihusisha na biashara haramu ya usafirshaji wa binadam waliokuwa wamewahifadhi katika nyumba ya mmoja wao iliyoko Muheza mkoani Tanga .


Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa uhamiaji mkoa wa Tanga Kagimbo Bakari amesema kuwa wamekuwa wakipambana kuweka mbinu mbalimbali kuweza kuwabaini wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo ambapo wamefanikiwa kuwakaata na tayari wamefikishwa mahakamani.


Amewataja mawakala hao kuwa ni Joseph Thimothi mwewnye nyumba walimokuwa wamehifadhiwa wahamiaji hao, wengine ni Charles Mwapela Kimaki Maneno, Athuman Mwameja pamoja Majoka Kipala wote hawa wakiwa ni raia wa Tanzania.


"Hawa ni mawakala ambao wanahusika na usafirishaji haramu wa binadamu karibu nyakati zote tumekuwa tukipambana kutafuta mawakala na tumewapata kutokana na mahusiano ya kesi ambazo nyingine ziko zinaendelea mahakamani na watuhumiwa wote tumewafikisha katika ofisi ya uhamiaji mkoa wa Tanga na mahojiano bado yanaendelea" alisema Kamanda Bakari


Aidha katika taarifa nyingine Jeshi la uhamiaji mkoa wa Tanga march 10, 2023 limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haram wanne raia wa Cameroon katika nyumba za kulala wageni jijini hapa wakidai kuwa wamekuja kwaajili ya kufanya mazoezi ya kujiunga na timu za Coastal Union na African Sports ambapo wameletwa na wakala wao aliyefahamika kwa jina la Benard Matomondo Mfaume.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa uhamiaji mkoa wa Tanga Kagimbo Bakari alieleza kuwa raia hao ambao waliingia hapa nchini kupitia uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA) na hatimaye kufanikiwa kupata visa ya matembezi (HV) za siku 90 badala ya visa za kibiashara (BV) kulingana na shughuli walizokuja kuzifanya.


"March10, 2023 usiku katika nyumba ya kulala wageni ya New MayLodge na New Palm Life zilizopo jiji la Tanga barabara ya 4 na 20 walikamatwa raia wanne wa Cameroon walikuja mkoa wa wanavyodai wao wamekuja katika timu za Coastal Union na African Sports kufanya mazoezi ili kujiunga na timu hizo kwa msaada wa wakala wao wa michezo aitwaye Benard Mtomondo Mfaume anaishi Dar es salaam"


"Uchunguzi wa awali unaonyesha raia hawa wa Cameroon waliingia kupitia uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere JKNIA na kupata viza za matembezi ya siku 90 na sio za kufanya shughuli zozote za michezo na wapo hapa tayari kwa kufanya mazoezi ili waweze kisajiliwa katika timu hizo za Coastal Union na African Sports" alisema Kamanda Bakari.


Hata hiyo kamanda huyo alibainisha kuwa mara baada ya kuwakamata raia hao waliwaita viongozi wa timu za African Sports na Coastal ambao walikanusha kutokuwatambua wala kuwa na mawasiliano nao na barua walizokuwa nazo zote ni za kughushi na paspoti walizokuwa nazo sio sahihi.


"Uchunguzi uliofanyika katika timu ya Coastal Union kupitia kwa katibu wa klabu anaeleza kutokuwatambua wala kuwafahamu na wala hana mawasiliano nao kwa mfano barua zote walizonazo ni za kughushi sii barua sahihi na paspoti walizo nazo sio paspoti sahihi kwa mujibu wa viongozi wa Coastal Union kwamba hawajawahi kuwaona wala hawahusiki nao"


"Kwa upande wa African Sports wao wameeleza kutokuwatambua na kwamba wana barua ya Fountain Get na Pamba Football klabu bado wakala wao wa michezo tunaendelea kumtafuta kwani hapokei simu ili tuweze kujua anaye wahudumia hapa mkoani Tang alielezaKamanda huyo.


Aliwataja majina raia hao kuwa ni Romanus Gwa, Cedric Donald Pouanguae Tchchoua, Sainsburunde Nji, pamoja na RowandBenard Messi Tangana.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top