Baadhi ya wakina Mama wa wilaya ya Longido |
Baadhi ya akina mama wakizungumza na wanahabari na kuomba kuwepo ulinzi wa kisheria katika eneo lililotengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo Yao |
Maipac team , Longido
Wafugaji wa wilaya ya Longido,mkoa Arusha wametaka ulinzi wa kisheria wa eneo la hekta186.794.2 walizotenga kwa malisho ya mifugo
Eneo la nyanda za malisho limetengwa na Vijiji 20 kati ya 49 wilayani Longido, ili kukabiliana na athari za Ukame na mabadiliko ya tabia tabia nchi.
Wakizungumza na waandishi wa habari wa kupitia mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa maarifa asilia unaofadhiliwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa(UNDP) kupitia programu ya miradi midogo walisema baada ya mvua kuanza kunyesha wanatarajia maeneo yao waliotenga kwa malisho kutovamiwa na kurejesha shida ya mifugo kufa kwa Ukame.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la wanahabari wasaidizi wa jamii za pembezoni MAIPAC, Mussa Juma akiwa katika majukumu ya kukusanya taarifa za maarifa ya asili katika kulinda nyanda za malisho longido |
Mradi huu unatekelezwa katika wilaya tatu za Longido,Monduli na Ngorongoro na shirika la wanahabari la kusaidia jamii za Pembezoni la (MAIPAC) kwa kishirikiana na CILAO na unataratibiwa na Jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF) .
Mfugaji Kileu Lipati alisema Wafugaji kwa kutumia maarifa Yao ya asili kwa kishirikiana na halmashauri ya Longido wameona ni bora kutenga maeneo ya malisho na kuwa na majani ya kutosha.
"Tunataka tutunze maeneo yetu wenyewe,kwa maarifa yetu ya asili ikiwepo kuwa na ratiba ya malisho ili kuruhusu mifugo kuhama kutoka eneo Moja hadi jingine "alisema
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Olbomba Kashira Alais alisema alisema wanaamini wakiachwa kutumia maarifa ya asili wanaweza kuendeleza ufugaji wa asili bila migogoro.
"Sisi sio waharibifu wa Mazingira kama ambavyo inasemwa sisi ni watunzaji wa mazingira ndio sababu katika maeneo yetu ndipo kuna wanyamapori wengi kwa kuwa kuna Mazingira mazuri "alisema
Mwenyekiti wa Kijiji Cha kimokowa wilaya ya Longido, Kilel Olenyokie Mollel akielezea eneo walilotenga kwa ajili ya malisho ya mifugo mbele ya wanahabari wa mazingira |
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimokowa wilaya ya Longido,Kilel Olenyokie Mollel alisema wameamua kutenga maeneo ya nyanda za Malisho ili kuyatunza kwa ajili ya ufugaji.
"Tumekuwa tukikabiliwa na Ukame katika wilaya yetu hivyo tumeona ni vizuri kutenga maeneo ya malisho ambayo hayatavamiwa"alisema
Baadhi ya wanahabari na watendaji wa shirika la Maipac na Cilao wakiwa makini kusikiliza umuhimu wa maarifa asili katika kutunza nyanda za malisho |
Neema Mollel mjumbe wa kamati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Longido,alisema ni muhimu wafungaji wa sera kuingiza maarifa ya asili katika sera zao kwani kutasaidia kupunguza migogoro ya wafugaji , wakulima na hifadhi.
"Hawa wafugaji wanapokuwa na uwezo wa kutumia vizuri ardhi yao kwa kuhama kufuata nyanda za malisho hakutakuwa na migogoro lakini maeneo Yao yakiendelea kuvamiwa na kupunguzwa kunaleta migogoro ikiwepo kuingiza mifugo hifadhini "alisema
Afisa mifugo na uvuvi wilaya ya Longido Nestory Daqarro akizungumza na wanahabari ofisini kwake |
Afisa mifugo na uvuvi wilaya ya Longido, Nestory Daqarro akizungumza na waandishi alisema wilaya hiyo, kutengwa maeneo ya malisho itasaidia wafugaji kupata malisho ya uhakika.
Daqarro alisema baada ya mashauriano na Vijiji na kutenga maeneo ya nyanda za malisho tayari serikali imeyatangaza rasmi maeneo hayo kama ni ya wafugaji na hivyo yatalindwa kisheria.
"Wasiwe ma hofu kuwa yatavamiwa haya ni maeneo yao na watayasimamia wenyewe kuhakikisha mifugo inapata malisho wakati wote na kuondoa adha ya mifugo kufa kwani mwaka huu zaidi ya mifugo 38,000 imekufa kwa ukame"alisema
Mradi wa uhifadhi Mazingira kwa maarifa ya asili ni sehemu ya miradi midogo 13 ambavyo inafadhiliwa na UNDP kwa kushirikiana na mfuko wa mazingira Dunia na Serikali ya Ujerumani.
Diwani mstaafu wa kata ya Manga akielezea umuhimu wa kuhifadhi maeneo ya nyanda za malisho |
Musa Murdoko ni mchungaji wa kanisa na Babtisti na mkazi wa kata ya Orbomba akielezea umuhimu wa kutengwa kwa nyanda za malisho |
Post a Comment