PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: CHEMCHEM CUP YATAMATIKA MAKLAYON WAJISHINDIA KOMBE NA KITITA CHA SHILINGI MILION MOJA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Timu ya Makilayon wakifurahia ubingwa wa chemchem Cup mara baada ya kushinda fainali ya michuano hiyo Mdorii wilayani Babati Wadhamini wa ...

 

Timu ya Makilayon wakifurahia ubingwa wa chemchem Cup mara baada ya kushinda fainali ya michuano hiyo Mdorii wilayani Babati



Wadhamini wa mashindano hayo wakikagua timu kabla ya kuanza kwa mchezo huo


Mwandishi wetu, Babati 

Timu ya soka ya Makilayoni FC  juzi imetwaa ubingwa wa michuano ya Chem chem CUP 2022 baada ya kuichabanga timu ya Mdori FC kwa penati 4-2  katika mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Mdori wilayani Babati, mkoani Manyara.

Katika mchezo huo, ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa Manyara, Makongoro Nyerere  hadi dakika 90 zilipomalizika timu hizo zilitoka zimefungana 1-1. 

Baada ya ushindi huo mabingwa hao ambao wametwaa mara mbili mfululizo mwaka2021 na 2022 walipewa zawadi ya fedha taslim sh 1 milioni kombe lenye thamani ya sh 1 milioni na Mpira.

Katika michuano hiyo ambayo mwaka huu lengo lilikuwa ni kupiga vita ujangili wa Twiga  jumla ya timu 16 zilishiriki  kutoka katika vijiji 10 ambavyo vinaunda Jumuiya ya Hifadhi ya wanyamapori ya Burunge(JUHIBU) 

Mdori FC walioshika nafasi ya pili walipewa zawadi ya Kombe na fedha taslim 500,000,Mpira ambapo awali timu zote 16 zilipewa seti ya jezi na mpira ili kushiriki michuano hiyo ikiwepo timu za mpira wa Pete.

Akizungumza katika michuano hiyo,Mkuu wa mkoa wa Manyara  Makongoro Nyerere aliwataka  vijana kushiriki katika kupambana na ujangili na kutunza Mazingira.

"Michezo hii sio tu ni fursa ya kukuza vipaji na kupata burudani lakini inalenga vijana kupambana na ujangili lakini pia kuhifadhi Mazingira"alisema

Meneja mahusiano wa taasisi ya Chemchem, Charles Sylvester ambayo imewekeza shughuli za Utalii wa picha na hoteli katika eneo hilo la JUHIBU alisema michuano hiyo tangu imeanzishwa miaka 10 iliyopita imekuwa na faida kubwa.

"Tumepata vipaji kuna wachezaji wametoka hapa wameenda ligi kuu lakini pia vijana wengi wamekuwa malinzi wa Wanyamapori na kupenda uhifadhi na tutaendelea kuiboresha"alisema

Mwenyekiti wa michuano hiyo, Belela Erasto alisema michuano ya mwaka huu imegharimu zaidi ya million 50 na alipongeza wawekezaji wa Chemchem kwa kuendelea kudhamini michuano hiyo kila mwaka.


Erasto alisema chemchem  waliowekeza  hoteli za kitalii na Kitalu Cha Uwindaji kupitia kampuni tangu za EBN na kufanya Utalii wa picha wamekuwa na manufaa makubwa katika wilaya ya Babati na mkoa mzima wa Manyara ikiwepo kutoa ajira zaidi ya 300 ,ujenzi wa shule,kusaidia sekta ya afya,maji na vikundi vya wanawake

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top