PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SERIKALI YASITISHA SHUGHULI ZA KIBINADAMU KATIKA MTO RUAHA MKUU (GREAT RUAHA)
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
      Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Dk.Seleman Jafo kwa niaba ya waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanza...

 

   

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Dk.Seleman Jafo kwa niaba ya waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wengine wa serikali waliposhuhudia kukauka kwa Mto Ruaha Mkuu (GREAT RUAHA)
Mkuu wa mkoa wa Iringa na Morogoro wakiwa na mkuu wa wilaya ya iringawaliposhuhudia kukauka kwa Mto Ruaha Mkuu (GREAT RUAHA)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Dk.Seleman Jafo kwa niaba ya waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kassim Majaliwa akiwa na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki alipowasili katika ofisi za Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

SERIKALI imewataka wananchi wote wanaofanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya Maji wasitishe shughuli mara moja kutokana na athari zinazoendelea katika Mto Ruaha Mkuu (GREAT RUAHA)  zinazosababishwa na kilimo,ukataji wa miti hovyo pamoja na ufugaji wa mifugo unaosababisha mto huo kukauka.

 

Akizungumza kwenye mkutano wa mawaziri nane uliofanyika Makao Makuu ya Hifadhi ya Ruaha iliyopo Msembe mkoani Iringa,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Dk.Seleman Jafo kwa niaba ya waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kassim Majaliwa alisema kuwa kukauka Mto Ruaha Mkuu (GREAT RUAHA)  umeathiri shughuli za kiuchumi ikiwemo mgao wa umeme pamoja kutokuwa na maji ya matumizi ya nyumbani katika mkoa wa Dar es Salaam

Dk.Jafo ameagiza bodi za bonde za maji na Baraza la Udhibiti na Usimamizi wa Mazingira kusimamia vyanzo vya maji kwa wale waliochepusha na wale wanaotumia maji kwa mujibu wa vibali kuangalia suala hilo.

Amesema kuwa suala la Ruaha tangu 1994 maji yanaacha kutiririka mwezi wa tano hiyo ni kutokana na shughuli za kibidamu kuendelea kwenye vyanzo vya maji.

 

Dk.Jafo alisema kwa kipindi hiki wanyama wakiwemo viboko,Mamba na aina mbalimbali za samaki wapo katika hali mbaya hivyo tuombe mvua zinyeshe kwa kipindi kifupi ili kuwaokoa wanyama hao waendelee kuishi vinginevyo watakufa.

 

“Mto Ruaha umekauka kabisa tulikuwa tukipita na helikopta kule juu mto umekauka kabisa mto huu hauna maji kabisa yanayotiririka hata ukienda Ihefu hali ni mbaya sana inaenda sambamba na kuathiri sekta nyingine


mfano mzuri sekta ya nishati mimi naaminiu kiwango cha umeme kinachozalishwa na maji leo hii inawezekana ukienda mtera naamini kiwango cha umeme kinachozalishwa katika mabwawa haya hali imekuwa ni mbaya sana” Dk.Jafo

 

alisema kuwa kupitia sheria ya maji ya mwaka 2022 Seleman Jafo aliwataka wakulima kuacha mara moja kulima na kuchepusha maji ya mto Ruaha kinyume na taratibu huku akiwataka kuondoka haraka na kuiagiza mamlaka ya bonde kusimamia sheria hiyo

 

Kwa upande wake Waziri wa Utalii Balozi Dkt.Pindi Chana alisema kuwa wananchi wanatakiwa kushikamana ili kulinda na kutunza maliasili zilizopo pamoja na vyanzo vya maji.


“Wote tulioingia hapa tumeshuhudia kwamba Mto Ruaha Mkuu (GREAT RUAHA) umeanza kukauka nitumie nafasi hii kuutangazia umma na watanzania wenzangu jukumu ni kutunza na kuendeleza maliasili kwa hiyo nawaombeni sana tushirikiane na kuendeleza hifadhi zetu na kuna vyanzo vya maji mengi sana vitasaidia idadi yetu kwa sensa ya mwaka huu maji haya pia yanasaidia hifadhi zetu”

 

Naye Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika la Taifa la Uhifadhi (TANAPA) William Mwakilema alisema ukame wa Mto Ruaha ni hatari kwa wanyama na hii ni kutokana bonde la Usangu/Ihefu kuendelea kwa shughuli za kilimo za kuzuia maji kwenye mto Ruaha.

 

Mwakilema amesema jitihada mbalimbali zinafanyika za kuweza Mto Ruaha kuwa na maji kwa vipindi vyote kutokana na mto huo kuwa na tegemeo kwa Taifa.

 

“Kipindi hiki ambacho mto umekauka ni kipindi kigumu kwa sababu wanyama wanataabika kupata maji wanyama kupata chakula maeneo ya kupumzika siyo mazuri lakini pia tunaona sisi ambao ni wasimamizi tunawakati mgumu pia kuangalia cha kufanya hali ya mto ruaha sio nzuri na jitihada mbalimbali zinapaswa kufanywa ili kuhakikisha huu mtoto unatirirsha maji vinginevyo uhai wa mto huu utakuwa mashakani “alisema Mwakilema

  

Kabla ya mkutano huo umechukua masaa matatu ya viongozi kujadiliana kutokana na hali waliokuta katika mto Ruaha ukiwa umekauka.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top