PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: NAIBU WAZIRI CHILLO ATAKA VIONGOZI KUTOA ELIMU YA UPANDAJI MITI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Khamis Hamza Chillo akizungumza  kwenye kikao na viongozi wa mkoa wa Rukwa wakati Kamati ya...

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Khamis Hamza Chillo akizungumza  kwenye kikao na viongozi wa mkoa wa Rukwa wakati Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta ilipotembelea mkoa huo kupeleka mrejesho wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 11 Oktoba 2022.

 Sehemu ya wajumbe wa Sekretarieti ya mkoa wa Rukwa wakiwa katika kikao cha  Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta mkoani Rukwa Oktoba 11, 2022.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete 

Naibu Waziri OR-TAMISEMI David Silinde

-Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Anthony Mavunde

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja

Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakiwasili katika kitongoji cha Kamkolwe kata ya Mpombwe Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa walipotembelea kitongoni hicho Oktoba 11, 2022

Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa kitongoji cha Kamkolwe kata ya Mpombwe Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa walipotembelea kitongoni hicho Oktoba 11, 2022

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Kamkolwe kata ya Mpombwe Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Oktoba 11, 2022 (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

 




Na Munir Shemweta, WANMM

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Khamis Hamza Chillo amewataka viongozi wa mikoa na wilaya nchini kutoa elimu ya upandaji miti kwa wananchi.

Aidha, ametaka viongozi hao kwenda kuelimisha wananchi namna bora ya kutunza vyanzo vya maji na kueleza kuwa changamoto kubwa iliyopo kwenye vyanzo hivyo ni shughuli kubwa za kibinadamu.

Naibu Waziri Chillo alitoa kauli hiyo mkoani Rukwa Oktoba 11, 2022 wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta kupeleka mrejesho wa Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.

Alisema, maeneo mengi yanayovamiwa wavamizi wake hawaendi tu kuvamia bali wanakata na miti na kuharibu vyanzo vya maji ambapo aliwataka viongozi wa mikoa na wilaya kuwaeleza wananchi ambao vijiji vyao vitabaki basi wapande miti.

"Watu waende kupata miti na si kupanda tu bali waishughulikie miti wanayoipanda". Alisema Chillo

Akigeukia suala la utumzaji vyanzo vya maji, alisema mbali na uchafuzi wa mazingira unaofanywa wenye maeneo yaliyovamiwa lakini wengine wanaharibu kabisa kwa kujenga nyumba na mwisho wa siku wanaharibu mazingira.

" Kikubwa sisi kazi tuliyokuwa nayo ni kwenda kuwaambia wananchi waende wakaheshimu na kutunza vyanzo vya maji na shughuli zetu za kibinadamu zisiharibu mazingira" alisema Chillo.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki aliwataka viongozi wa mikoa na wilaya kutekeleza na kumaliza kazi iliyo mbele ya kushughulikia changamoto za ardhi Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iendelee na mambo mengine.

"Tusimsoneneshe rais kwa kuanzisha migogoro mingine maana atasikitika sana kwamba ametoa rasikimali fedha, watu na muda kumaliza migogoro halafu tuanzishe kamati nyingine na tujitahidi kuanzia ngazi ya chini ili kudhibiti migogoro inayoweza kutokea katika maeneo mengine"

Ridhiwani Kikwete Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka watendaji wa sekta ya ardhi kuacha nidhamu ya woga kwa kutekeleza maelekezo ya wanasiasa bila kufuata taratibu.

"Wataalamu wetu waelekezeni viongozi wa siasa taratibu za kupata maeneo, mkituachia sisi tukioongoza harakati mwisho wa siku mnatengeneza hapa maeneo yote kuvamiwa na hakuna taratibu halafu mtakuja kusema walikuwa viongozi hawakufanya lolote kumbe wewe mwenyewe ni sehemu ya uvurugaji" alisema Ridhiwani.

Kwa upande wake Naibu Waziri OR- TAMISEMI David Silinde alisema ofisi yake kwa sasa haitasajili kijiji au maeneo ya utawala bila kushirikiana na wizara nyingine za kisekta kwa lengo la kujua kama maeneo hayo hayako kwenye hifadhi au eneo oevu sambamba na kupata mapendekezo ya mipaka kutoka wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi.

Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde aliwataka viongozi katika mikoa kuhakikisha kunakuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi hasa kupanga maeneo ya kilimo na wizara yake kwa sasa iko kwenye mchakato wa kutunga sheria ya kilimo ili kutunza maeneo yanayofaa kwa kilimo na kutumika kwa kazi hiyo.

" hivi sasa tuna ushirikiano mzuri na wizara ya ardhi yale maeneo yote yanayobainika kufaa kwa kilimo tu nuyagazette ili kuwa na ulinzi wa maeneo hayo na mwisho wa siku pasiwepo tunataka pasiwepo muingiliano wa matumizi ya ardhi na tunaamini kupitia mkakati huu tutapunguza changamoto kubwa ya wakulima na wafugaji" alisema Mavunde.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja alieleza kuwa, changamoto kubwa katika uhifadhi ni muingiliano wa shughuli za binadamu na hifadhi na kuwaomba viongozi kushiriliana na kwa kusimamia kila mtu akasimamie eneo lake na kusisitiza kuwa wakifanya hivyo basi migogoro itaisha.

" tukiwapa maelekezo ya kutosha na kusimamia hatutafika hapa tulipofika na hii jamani tukitoka humu kila mtu akielewa tiyokubaliana akatekeleze" alisema Masanja

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top