Na: Mwandishi wetu, Manyara
Jumla ya timu 20, zinatarajiwa kushiriki ligi ya Chem Chem CUP,
wilayani Babati mkoa wa Manyara ambapo zawadi zenye thamani ya sh 4.5
milioni zitatolewa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mratibu wa ligi hiyo, ambayo hufanyika
kila mwaka,katika uwanja wa Mdori, Charles Godluck alisema, lengo lake
ni kupiga vita ujangili na kuhamamisha jamii uhifadhi za mazingira.
Godluck
alisema, ligi ya chem chem CUP,mwaka huu inatarajwa kufunguliwa na Mkuu
wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, Agosti 19 na itatanguliwa na
mkutano wa kutolewa jezi wa timu zote agosti 10 mwaka huu.
"hivi
sasa tumezitaka timu zote ifikapo Agosti 4 ziwe zimethibitisha lakini
pia kujitokeza kwenye kikao cha kupanga ratiba Agosti 10"alisema
Alisema
mwaka huu bingwa wa soka, atapewa zawadi ya fedha taslimu 1.7 milioni
na kombe,mshindi wa pili fedha 1.1 milioni, wa tatu 600.000 na wa nne
300,000.
"pia kutakuwa na zawadi wa kocha, bora, timu bora na mchezaji bora"alisema
Alisema
katika michuano hiyo, pia kutakuwa na michezo kwa wasichana ambapo,
bingwa atazawadiwa 400,000 na pia kutakuwa na ngoma za kitamaduni na
michezo mingine.
Meneja
wa taasisi ya Chemchem Foundation, Recardo Tossi, ambao wamewekeza
ujenzi wa hoteli katika eneo la Mdori, alisema ligi hiyo, imekuwa
ikishirikisha zaidi ya wanamichezi 400 na kuwa na ufanisi mkubwa.
"tunataka
jamii ambayo inazunguka kijiji cha Mdori na tarafa nzima ya Mbugwe na
wilaya ya babati, kuwa wahifadhi wazuri na kupiga vita ujangili"alisema
Na hapa chini ni baadhi ya matukio katika picha ya michuano iliyofanyika mwaka jana ambapo timu ya mdori fc ilijinyakulia kombe la michuano hiyo.
Post a Comment