Wakili wa Serikali, Costanine Kalula amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo limeitishwa ili Wema na wenzake waanze kujitetea, lakini Wema anaumwa, hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Baada ya kueleza hayo, Mama mzazi wa Wema Sepetu, Miriam Sepetu aliieleza mahakama kuwa Wema alifika mahakamani hapo lakini wakati anasubiri kuingia mahakamani alianza kuumwa ambapo alianza kutapika na hivyo kuondoka.
Baada ya maelezo hayo , Hakimu, Thomas Simba ameahirisha kesi hiyo hadi May 29 na 30, 2018 ili washtakiwa watakapoanza kujitetea.
Mbali na Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.
Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kuzitumia.
Inadaiwa February 4, 2017 katika makazi ya Wema eneo la Kunduchi Ununio, washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.
Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa February mosi 2017 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.
Post a Comment