Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair Ltd ,Tom Kunkler akizungumza mbele ya waandishi kuhusu tukio la Maonesho ya Kimatifa ya Utalii ya KAribu Kilifair yanayotaraji kufanyika mjini Moshi ,June 1 hadi 3 mwaka huu.
Viongozi wa Kampuni ya uokoaji ya Kilimanjaro SIR wakifuatilia maelezo juu ya manesho hayo yaliyokuwa yakitolewa kwa wanahabari.
Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Kilifair inayoratibu maonesho ya Karibu Kilifair ,Dominic Shoo akizungumzia tukio hilo kubwa la Kitalii.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uokoaji ya Kilimanjaro SIR ,Ivan Brown akizungumza wakati wa kikao na wanahabri kuhusu tukio hilo.
Meneja Mauzo wa Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines ,Fitsimt Dejene ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Maonesho ya Kimataifa ya Karibu Kilifair yanayotaraji kufanyika mjini Moshi.
Waratibu wa Maonesho ya Karibu Kilifair wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadhamini wa maonesho hayo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
MAKAMPUNI 380 yanayojishughulisha na Utalii yanataraji
kushiriki Maonesho ya Kimataifa ya Karibu Kilifair huku kampuni ya Kilifair Ltd
inayoratibu maonesho hayo ikitangaza kuandaa safari za kifamilia
zitakazoshirikisha watu kutoka nchi mbalimbali Duniani kujionea vuvitio vya
utalii kwa lengo la kuvitangaza kimataifa.
Maonesho ya kimataifa ya Utalii yaliyopewa jina la Karibu
Kilifair yanafanyika kwa mwaka wan ne sasa yakiwakutanisha wadau mbalimbali wa
sekta ya Utalii wa Tanzania na nje ya nchi ,kwa lengo la kutangaza bidhaa
mbalimbali za Utalii ikiwemo vivutio mbalimbali.
Kwa mara ya kwanza Kampuni ya Kilimanjaro SIR
inayojishughulisha na ukoaji wa wageni waliopata matatizo katika maeneo yenye
miinuko kama Mlima Kilimanjaro na Meru inataraji kushiriki katika maonesho hayo
huku Shirika la ndege la Ethiopian Airlines likitangaza kutumia maonesho hayo
kutangaza vivutio vya Utalii kwa wageni watakaosafiri na ndege wa shirika hilo.
Maonesho ya Karibu Kilifair yanayoratibiwa na Kampuni ya Kilifair
Ltd awali yalijukiana kama Kilifair yakidhaminiwa na Kampuni mbalimbali za
ndani na nje ya nchi .
Post a Comment