PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BAVICHA YAFUKUZA UANACHAMA VIONGOZI WAKE WAWILI LEO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Baraza kuu la Vijana Chadema taifa limewafukuza uanachama wanachama  Getrude Ndibalema aliyekuwa naibu katibu mkuu wa baraza hil...
Baraza kuu la Vijana Chadema taifa limewafukuza uanachama wanachama  Getrude Ndibalema aliyekuwa naibu katibu mkuu wa baraza hilo na Dickson kibona aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kilimanjaro kwa kosa la usaliti ndani ya chama.

Akiongea na wanahabari Patric Ole Sosopi  Mwenyekiti wa baraza hilo amesema kuwa wamefikia hatua ya kuwafukuza uwanachama watu hao baada ya uchunguzi kufanyika na kubainisha  kuwa wana makosa ya usaliti ambapo hivyo kwanzio Leo may 21 sio wanachama wala Viongozi wa chama hicho.

Ameeleza kuwa pia baraza hilo limemchagua Baraka Mfilinge  Mwenyekiti wa baraza hilo Mkoa wa Iringa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa baraza hilo.

Amesema wametafakari hali ya kisiasa nchini na wameweza kugundua kuwa kuna mkwamo wa demokrasia hapa nchini..

Pia wamelitaka Jeshi la Polisi kujitokeza hadharani na kutangaza kuwa wameshindwa kuwakamata watu waliofanya tukio la kumpiga   Mbunge Tundu Lissu na waruhusu vyombo vya uchunguzi vya kimataifa kufanya kazi hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top