PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: RC GAMBO AAGIZA KILA HALMASHAURI ARUSHA KUPANDA MITI MILIONI 1.5 KWA MWAKA KUTUNZA MAZINGIRA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mgeni rasmi wa shughuli hiyo Mkuu wa Wilaya ya Karatu,Theresia Muhonga aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Baadhi ya...
Mgeni rasmi wa shughuli hiyo Mkuu wa Wilaya ya Karatu,Theresia Muhonga aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo

Baadhi ya washiriki waliohudhuria



Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya umeme jua ya mobisol waliposhiriki katika shughuli hiyo

Baadhi ya washiriki wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya karatu  Theresia Muhonga juu ya agizo lililotolewa na mkuu wa mkaoa wa Arusha Mrisho Gambo juu ya kupanda iti milioni 1.5 kwa kila halmashauri
 
NA: ANDREA NGOBOLE, PMT

Mkuu wa mkoa Arusha,Mrisho Gambo ameagiza halmashauri zote za mkoa Arusha kupanda miti 1.5 milioni kwa mwaka ili kutunza mazingira.
Gambo alitoa hutuba hiyo kwenye maadhimisho ya upandaji miti mkoa Arusha ambayo yalifanyika kijiji cha Selela wilaya ya Monduli.

Katika hutuba ya Gambo ambayo ilisomwa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu,Theresia Muhonga alisema ili kufanikisha hilo,kila halmashauri inapaswa kutenga fedha kila mwaka.

"Tengeni fedha kila mwaka kusaidia kupanda miti na kuihifadhi" alisema
Mkuu huyo wa mkoa alizitaka halmashauri kushirikiana na wadau mbali mbali ili kufanikisha hilo zikiwepo sekta binafsi.

Awali Meneja Masoko wa kampuni ya Mobisol,David Ngwale ambao walikuwa sehemu ya wadhamini wa zoezi hilo,alisema suala la utunzwaji mazingira ni la watanzania wote.

Alisema kampuni yao ambayo huzalisha umeme wa jua itaendelea kusambaza huduma huyo hasa maeneo ya vijijini ili kuzuia uharibifu wa mazingira katika kupata nishati ya umeme.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli,Stivin Ulaya alisema wilaya hiyo kwa kushirikiana na wadau ikiwepo Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imejopanga kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

"Tumekuwa na miradi ya kupanda miti,kuhimiza majiko sanifu na tunashukuru wadau kama Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro kusaidia" alisema.

Meneja wa malisho ya wanyama katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Hillal Mushi alisema Mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na serikali  misitu na kulinda vyanzo vya maji.

Alisema NCAA pia imekuwa na miradi ya kusambaza miti bure vijijini ili kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top