PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: UWT MKOA WA ARUSHA WATAKIWA KUONDOA MAKUNDI NA MAKOVU YA UCHAGUZI ILI KUJENGA JUMUIYA HIYO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT mkoa wa Arusha Yasmini Bachu amewataka wanawake wa jumuiya hiyo kuvunja makundi yaliyokuw...

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT mkoa wa Arusha Yasmini Bachu amewataka wanawake wa jumuiya hiyo kuvunja makundi yaliyokuwepo kipindi cha uchaguzi na kushirikiana kwa pamoja ili kujenga chama na jumuiya hiyo.

Ameyasema hayo kwenye baraza la wanawake wa wilaya ya Arumeru ambapo amesema kuwa yeye kama kiongozi wa wanawake aligombea na wenzake lakini akapata nafasi hiyo sasa kilichobaki ni kuungana na kuwa wamoja kwa kuwa lengo ni kushinda chaguzi zinazokuja

Pia amesisitiza jambo hilo lifanyike mpaka ngazi ya vikao kwenye wilaya kwasababu walikula kiapo cha kuleta maendeleo kwa jamii na kushirikiana kwa kila jambo na kila mtu afanye kwa dhati ya moyo wake.

Pamoja na hayo ameitaka jumuiya hiyo kulipa kodi katika miradi yake kwa kuwa wanakusanya fedha kutokana na miradi hiyo kwasababu hakuna maendeleo bila kulipa kodi

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top