PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MHADHIRI WA SHERIA CHUO KIKUU CHA DARESALAAM AMPA RAISI MAGUFULI MBINU ZA KUPATA KATIBA MPYA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt James Jasse amemshauri Raisi wa jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Do...



Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt James Jasse amemshauri Raisi wa jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dokta John Magufuli kutumia njia ya kuunda kamati ya wataalamu ambayo haifungamani na upande wowote kukaa ili kuona jinsi ya kupata katiba mpya.
Akitoa mada katika semina iliyoandaliwa na kituo cha Sheria na haki za Binadamu LHRC  kwa waandishi wa habari wa radio za jamii mkoani Dodoma Dokta Jesse amesema kuwa Njia ya Kutumia Kamati ya Wataalamu gharama yake ni ndogo kuliko kuitisha tena upya Bunge la Katiba.
 Dr. JESSE akiwasilisha mada yake mbele ya wanahabari wa radio za kijamii katika semina hiyo
 
  Katika mafunzo hayo yaliyokuwa yanajenga uelewa kwa wanahabari kuhusu sheria ,haki za binadamu na mchakato wa katiba mpya kwa pamoja yaliyofanyika mkoani humo, amesemakuwa suala la katiba ni muhimu kwakuwa ni jambo ambalo litatumika sasa na katika vizazi vingine vijavyo pia.
Amesema kuwa kamati hiyo itakuwa na faida kubwa kwasababu itaangalia kilicho bora kwa kuzingatia Sera za Nchi pamoja na kupewa Hadidu za Rejea ambapo pia alitolea mfano wa nchi ya Kenya ambao walitumia njia hiyo ya kamati maalum kupata katiba mpya inayotumika sasa.
“Hii Kenya walifanya baada ya kuwa kuna draft ile ya wananchi unadraft ile ya serilaki wakatengeneza commete of experts wakawambia sasa nyie tunawapa hadidu za rejea muangalie mazuri yaliyoko pande zote mtutengenezee draft nzuri halafu tutaipeleka kwa wananchi kwa hiyo wale wana harmonize na kureconcile rasimu ya warioba na katiba inayopendekezwa na hata katiba hii ya 1977 itakuwana document mbayo itakuwa ni high Brid ina pande zote lakini hili nalo litakuwa ni utashi na nadhani hii ni approach ambayo nadhani Raisi wetu ataipenda na itapunguza gharama yake itakuwa ndogo”Alisema Dkt Jesse
Ameongeza kuwa namna ya kuipata kamati hiyo ya wataalamu hao ni kuchagua watu wasioegemea upande wowote na wajiite jina ambalo wanaweza kutumia katika mchakato huo ili kuwapeleka wananchi kwenye kura ya maoni na kuipitisha kwa kuikubali au kuikataa baada ya kushirikisha rasimu za katiba zote. Naye afisa msaidizi kutoka kitoka kituo cha sheria na haki za binadamu waliowezesha mafunzo hayo amesema kuwa wameamua kuchagua radio jamii kwasababu ndizo zinazosikilizwa zaidi na watu wa vijijini ili kupata uelewa juu ya mchakato wa katiba mpya.
Amesema kuwa watu wengi walioko vijijini hawajui masuala ya sheria na katiba lilikuwa ni jambo ambalo linapotea kwenye masikio ya watu hivyo wakaona ni vema kuibua kupitia waandishi wa habari ambao wanawagusa wananchi moja kwa moja
Akizungumza katika semina hiyo meneja wa Radio ya Unyanja Fm Patrick Kosima amesema kuwa wao kama wanahabari semina hiyo wamepata ufahamu na watapata fursa ya kuandaa vipindi mbalimbali ambavyo vinahusu katiba kwa kuwa wametambua sualala mchakato huo ni wapi ulikwama ili waanze kutoa ufahamu kwa watu wengine
Pia Kosima ameishauri serikali ichukue nafasi yake juu ya kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mchakato wa katiba mpya kwa kuwa kwasasa imekaa kimya licha ya kwamba kuna mambo mazuri yanafanyika lakini siyo mbadala wa katiba mpya.
Kwa upande wake Ashura Mohameni Mwandishi wa habari kutoka Radio 5 Arusha amesema kuwa kupitia mafunzo hayo yamewasaidia kupata uelewa wa namna ya kusaidia wananchi kuhusu katiba naye Paulina Mpiwa kutoka Baloha Fm amesema kuwa yeye alikuwa anashindwa ataanzia wapi lakini kwasasa atajua jinsi ya kuongelea suala hilo katika vipnindi vyake radioni hapo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top