Kikosi cha Liverpool kimeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace iliyokuwa Uwanja wake wa nyumbani, Selhurst Park, jioni hii.
Palace ndiyo walikuwa wa kwanza kujipatia bao la kwanza kwa njia ya penati kunako dakika ya 13 ya mchezo likifungwa na Luka Milivojevic. Penati hiyo ilisababishwa na Mlinda Mlango wa Liverpool, Loris Karius baada ya kumdondosha Wilfried Zaha kwenye eneo la hatari.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, Palace walikuwa mbele kwa bao hilo moja la penati.
Kipindi cha pili kilianza kwa kuchukua dakika tatu pekee, ambapo Msenegal, Sadio Mane aliipatia Liverpool bao la kusawazisha na kuufanya mchezo huo kuwa 1-1.
Na kuelekea mwishoni mwa mchezo zikiwa zimesalia dakika 6 mpira kumalizika, Mohamed Salah alipachika bao la pili na mpaka mechi inakwisha Liverpool walikuwa mbele kwa mabao hayo mawili kwa moja.
Matokeo hayo yanaifikisha Liverpool mpaka nafasi ya 3 kwa kujikusanyia alama 66 ikiwa ikiwa imecheza michezo 32, nyuma ya Tottenham yenye alama iliyocheza mechi 30.
Post a Comment