PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: DR. MWAKYEMBE AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI, MAWASILIANO NA UHUSIANO SERIKALINI JIJINI ARUSHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
WAZIRI wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo ,Dkt Harson Mwakyembe amewaagiza Maafisa Habari wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa ...




WAZIRI wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo ,Dkt Harson Mwakyembe amewaagiza Maafisa Habari wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria,Kanuni na Taratibu za serikali huku akiwataka kuzingatia malengo ya kitaifa waliyojiwekea katika kikao kilichopita.

Mbali na agizo hilo Dkt Mwakyembe pia amesema serikali haita wavumilia maafisa habari ambao hawatambui wajibu wao  huku akiwafananisha na maafisa habari hewa  ambao wanageuza tovuti za Serikali kuwa magofu badala ya kuwa na habari mbalimbali zenye tija na maendeleo kwa taifa la Tanzania.

Dkt Mwakyembe ameyasema hayo leo wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikali ,kinachofanyika katika Ukumbi wa mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha kinachowakutanisha zaidi ya Maafisa Habari zaidi ya 300 kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katika kikao hicho kinachoenda sambamba na Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO)kinafanyika wakati kukiwa bado kuna changamoto katika kada ya maafisa Habari wa taasisi za Umma ikiwemo uharaka wa ufikishaji wa taarifa za serikali kwa umma .

Katika mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ,Dkt Hassan Abbas amewakumbusha washiriki wa mkutano huo kuenenda kimkakati huku akitoa nukuu za mcheza filamu Mashuhuri nchini Marekani ,Anord Schwazniger .
Naye Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ,Tanzania ,Alvaro Rodriguez amesema serikali ina umuhimu mkubwa wa kufundisha na kuhabarisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia zinazo iunganisha Dunia .

“Umoja wa Mataifa unaiona Tanzania ya leo na kesho yenye mafanikio mengi sana,Demkorasia ,kufikia uchumi wa kati ,Elimu Bure,kupiga vita rushwa ni kati ya vitu vinavyoipa Tanzania sifa ya nchi iliyo tayari kuleta maendeleo ya nchi kwa ajili ya wananchi.”alisema Rodriguez.

Katika mkutano huo TAGCO ambacho ni chama kisicho cha kiserikali (NGO) kikiwa na madhumuni ya kukuza Mawasiliano na kuongeza Usambazaji wa  Taarifa ndani ya serikali na kati ya serikali na Wananchi  kimekabidh vyeti kwa Wadhamini wa mkutano huo.





Mwenyekiti wa chama cha maafisa habari, mawasiliano na uhusiano serikalini ndugu Pascal Shelutete
ambaye pia ni Meneja Mawasiliano Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) akiwakaribisha maafisa hao katika kikao kazi kilichoanza leo katika ukumbi wa AICC na kutambulisha mada, watoa mada na mgeni rasmi na wageni waambata walisohririki katika kikao kazi hicho na utoaji zawadi kwa wafadhili waliowezesha mkutano huo kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mataifa cha Arusha (AICC).






Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakati wa ufunguzi mkutano wa 14 wa kikao kazi cha Maafisa hao kilichoanza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi, 2018 Jijini Arusha.






Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi akizungumza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakati wa ufunguzi mkutano wa 14 wa kikao kazi cha Maafisa hao kilichaonza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi,2018 Jijini Arusha.






Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gabriel Daqqaro akuzungmza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakati wa ufunguzi mkutano wa 14 wa kikao kazi cha Maafisa hao kilichaonza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi,2018 Jijini Arusha.




Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akifurahia jambo na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini , Alvaro Rodriguez wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kilichaonza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi,2018 Jijini Arusha.




Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Elishilia Kaaya mara wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kilichaonza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi,2018 Jijini Arusha.




Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akimkabidhi cheti cha shukrani ya udhamini wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini, Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt. Jimmy Yonas wakati wa kutoa vyeti kwa wadhamini wa kikao kazi hicho kilichaonza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi,2018 Jijini Arusha.




Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt Jimmy Yonas akizungumza jambo na aliyekuwa kuwa Katibu wa Hayati Baba wa Taifa, Mzee Kasoli wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kilichaonza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi,2018 Jijini Arusha.




Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kilichaonza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi,2018 Jijini Arusha.




Baadhi ya Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakipata maelekezo kuhusu taratibu mbalimbali za usajili katika mkutano wa 14 wa kikao kazi chao kilichoanza leo Jumatatu Machi 12-16 Jijini Arusha.




Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadues akimwongoza Mhariri Mtendaji wa Makampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt. Jimmy Yonas kuelekea katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano huo leo Jumatatu Machi 12, 2018 katika ukumbi wa kituo cha Mikutano cha Kimataifa wa Arusha.




Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadues akimwongoza Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) Alvaro Rodriguez kuelekea katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano huo leo Jumatatu Machi 12, 2018 katika ukumbi wa kituo cha Mikutano cha Kimataifa wa Arusha
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe wanne kutoka kushoto akiwa pamoja na baadhi ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO), mara baada ya kufungua Kikao kazi cha 14 kinachoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akifungua Kikao Kazi cha 14 cha Maofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini zaidi ya 300 wanaokutana katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC)

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), nchini Tanzania Alvaro Rodriguez akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha maofisa Maofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini zaidi ya 300 wanaokutana katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC)

Katibu Mkuu Wizara ya Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Suzani Mlawi akizungumza na Maofisa Habari, Mawasiliano na Uhusino Serikalini wakati wa kikao kazi cha 14 kinachoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC)


Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kinachotajwa kama Kikao kazi wakifuatilia kwa karibu Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbas akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha 14 cha Maofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC)

Mwenyekiti wa Chama cha Maofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO),ambaye ni Meneja Mawasiliano Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Paschal Shelutete akizungumza wakati wa utoaji zawadi kwa wafadhili waliowezesha mkutano huo kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mataifa cha Arusha (AICC)

Afisa habari na mawasiliano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), Walter Mairo akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania Alvaro Rodriguez wakati wa upokeaji vyeti kutoka kwa wafadhili wa Mkutano wa Maofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano (TAGCO), katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Afisa habari na mawasiliano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), Walter Mairo akipokea Cheti kwa niaba ya Mhifadhi Mkuu wa NCAA Dk. Freddy Manongi kutoka wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe ikiwa ni heshima ya kutambua mchango wa Mamlaka kufadhili Mkutano wa 14 wa Maofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unafanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Mmoja wa wawakilishi wa Mashirika yaliyofadhili mkutano huo akipokea Cheti kutoka wa Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akibonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Tovuti ya TAGCO (www.tagco.go.tz), tovuti hiyo imelenga kuimarisha shughuli mbalimbali za Chama hicho

Mwenyekiti wa TAGCO Paschal Shelutete (kulia), akiwaongoza wageni waalikwa kuingia katika ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), tayari kwa ufunguzi wa kikao kazi cha 14 cha Maofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano, kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Arushaa Gabriel Daqarro, Waziri wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbas

Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kinachotajwa kama Kikao kazi wakifuatilia kwa karibu Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top