Maamuzi ya viongozi hao yametokana na kile wanachodai kuwa vyama vyao vimehama kutoka kuwa taasisi za umma na kuwa kampuni za watu binafsi na wapambe wao, aidha, viongozi hao wamekiri kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Awamu ya Tano na wameguswa na Mageuzi makubwa yanayofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kipindi hiki.
Mmoja wa viongozi hao, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo, Ndugu Kansa Mohammed Mbaruku amefafanua kuwa maamuzi hayo ya kukihama chama cha ACT na kujiunga na CCM ni kutokana kuwepo na ugonjwa mkubwa sana uliyopo kwenye vyama vya upinzani, wa kutokutembea kwenye maneno na misingi yake, vinasema ni vyama vya kidemokrasia ila havina demokrasia kabisa na mambo mengi yanakwenda kinyume na misingi ya uanzishwaji wa vyama hivi na jambo hili linawakatisha tamaa wanachama wengi wa vyama hivi
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wa Chadema waliohamia CCM, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Siha, Ndg. Daniel Nkini amesema wamegundua Chama cha Mapinduzi katika masuala ya maendeleo hakibagui wananchi tofauti na ambavyo vyama vingine vimekuwa vikitenda.
Katibu wa Itikadi na Uenezi ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi amewapokea viongozi hao waliokuwa wa vyama vya upinzani, amewahakikishia wamefanya uamuzi sahihi, wamechagua upande mzuri na washirikiane na wanachama wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukijenga chama na nchi ya Tanzania.
Ndugu Polepole amewaapisha wanachama hao, Katika kiapo cha Imani na Ahadi za mwanachama wa CCM na akisisitiza umuhimu wa wanachama wapya na wale wazamani kujengeka kiitikadi na kiimani ya Chama na kuishi sawasawa na Imani, Itikadi na Ahadi za mwana CCM huku akinukuu usemi maarufu wa “Imani bila matendo imekufa”.
Huu ni muendelezo wa mamilioni ya watanzania wanaojiunga na CCM na mamia ya viongozi wa vyama vya upinzani kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika awamu hii ya tano chini ya uongozi wa Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
MOSHI, KILIMANJARO
Post a Comment