Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya
Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibok akizungumza katika hafla fupi
ya kuagwa kwa wazelendo 47 waliopanda mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya Washiriki katika changamoto ya kupanda Kilimanjaro kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Ndani na utunzaji wa Mazingira.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za
Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza katika hafla ya kuwaaga
washiriki wa changamoto ya upandaji wa mlima Kilimanjaro kwa ajili ya
kutangaza Utalii wa ndani na Utunzaji wa Mazingira.
Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii
Tanzania ,Balozi Charles Sanga (kulia) alikua ni miongoni mwa Wazalendo
walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimajaro.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara anayeshiriki
zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mara ya 10 sasa akazungumza na
washiriki wa zoezi hilo kabla ya kuianza safari.
Mkuu
wa wilaya ya Rombo ,Agness Hokororo ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika
hafla ya kuwaaga Wazalendo 47 kupanda mlima Kilimanjaro.
Mkuu
wa Wilaya ya Rombo ,Agnes Hokororo akimkabidhi Bendera ya taifa Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,Jenerali George Waitara kabla ya kuanza kwa
safari hiyo.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,Jenerali George Waitara akikabidhi Bendera
kwa Mkuu wa kamandi ya Brigedi ya Magharibi,Brigedia Jenerali Mkumbo
aliyekuwa mkuu wa Msafara wa Wazalendo 47 waloshiriki kupanda Mlima
Kilimanjaro.
Wazalendo
47 walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro wakiwa katika
picha ya pamoja na mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Rombo .Agness Hokororo.
Safari katika siku ya kwanza ya kuelekea kilele cha Uhuru ikaanza ,Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali ,Georg Waitara akiongoza.
Uzalendo wa kuifikisha Bendera ya Taifa katika kilele cha Uhuru ndio uliongeza morali kwa washiriki ya kuendelea na safari .
Wazalendo walipata mapumziko katika eneo la Nusu njia lijulikanalo kama Kisambioni na baadae kuendelea na safari.
Safari
ya Wazalendo haikuwacha nyuma ,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro ,Betrita Loibook na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi
za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete .walitembea licha ya kunyeshwa na
mvua.
Hatimae
safari katika siku ya kwanza kwa Wazalendo 47 kuelekea kilele cha Uhuru
ikakamilika mara baada ya kuwasili kituo cha mapumziko cha Mandara.
Post a Comment