Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano
wa Kwanza kwa makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya nyanda
za juu kusini kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi ambao
umefunguliwa rasmi, Jana Novemba 21, 2017. Picha Zote Na Mathias CanalNaibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano
wa Kwanza kwa makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya nyanda
za juu kusini kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi ambao
umefunguliwa rasmi, Jana Novemba 21, 2017. Makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya nyanda za juu kusini wakifatilia hotuba ya Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi ambao umefunguliwa rasmi, Jana Novemba 21, 2017. Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akifatilia mada mbalimbali kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi Mara baada ya kufungua Mkutano wa Kwanza kwa Makatibu Tawala na washauri wa Kilimo wa Mikoa ya nyanda za juu kusini, Jana Novemba 21, 2017.Makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya nyanda za juu kusini wakifatilia hotuba ya Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa bei elekezi ambao umefunguliwa rasmi, Jana Novemba 21, 2017.
Na Mathias Canal, Mbeya
Makatibu
tawala kote nchini wametakiwa kutafiti na kubaini wafanyabiashara
wadogo wa mbolea wanaokiuka bei elekezi kutokana na wafanyabiashara
wakubwa kuwauzia wafanyabiashara hao wadogo kwa bei elekezi ya rejereja
badala ya bei ya jumla.
Mwito
huo umetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa
wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza kati ya mikutano
saba (7) katika Kanda saba (7) za kilimo nchini inayotegemewa kufanyika
ambao ni muhimu kwa makatibu tawala na washauri wa kilimo wa mikoa ya
nyanda za juu kusini wa kuelimishana kuhusu ubora wa mbolea na mfumo wa
bei elekezi ambao umefunguliwa rasmi.
Mhe
Naibu Waziri wa Kilimo aliwasihi Makatibu Tawala hao wa Mikoa na
wataalamu wa kilimo kuhakikisha kwamba wanasimamia bei elekezi ya
mbolea, Wanatoa Elimu kwa Wakulima ili wanunue mbolea bora na pia
kuimarisha vikundi vya wakulima ili waweze kutumia nguvu ya umoja katika
kuboresha kilimo kwa ajili ya utoshelevu wa mahitaji ya kaya zao na
kuuza ziada hapa nchini na nchi za nje.
Alisema
kuwa wafanyabiashara licha ya kufahamu kuwa wanatakiwa kugawana faida
na wauzaji wa rejareja lakini bado wanakiuka taratibu za kisheria hivyo
aliwaagiza kuacha tabia hiyo ili mawakala wauze kwa rejareja na kwa bei
elekezi bila kuathiri biashara zao.
Alisema
Katika Sekta ya Kilimo mbolea ni moja ya pembejeo zinazohitaji
ushirikiano mkubwa kutokana na ukweli kwamba inahitajika kwa wingi na
ina gharama kubwa, inahitaji utaalamu katika matumizi yake na kwamba ni
bidhaa inayoharibika kwa haraka endapo viwango vya utunzaji wake
havizingatiwi.
Mhe
Mwanjelwa aliwaagiza wakaguzi wote wa mbolea nchini kufuatilia na
kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara wa mbolea ana leseni ya kufanya
biashara ya mbolea ambayo itatolewa bure na TFRA na pia wahakikishe
kwamba wote wamepata mafunzo haraka iwezekanavyo.
“Mbolea
ni moja ya vichocheo vikubwa sana katika suala hili na hivyo, mwisho wa
mkutano huu tunategemea kupata taarifa ya mikakati ya namna Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa zitakavyosimamia ubora na bei elekezi ya
mbolea ili Mkulima aweze kuipata na kuitumia kwa lengo linalokusudiwa”
Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Naibu
Waziri huyo alisema kuwa Wizara ya kilimo ilitunga Kanuni ya Ununuzi wa
Mbolea kwa Pamoja (Fertilizer Bulk Procurement Regulations) na
kuzitangaza kwenye Gazeti la Serikali kupitia tangazo G.N. 49/2017.
Pamoja na kuunda kanuni hizo, Wizara ya kilimo ilirekebisha Kanuni ya
Mbolea ya mwaka 2011 kwa Kanuni zilizotangazwa katika Gazeti la Serikali
kwa tangazo G.N. Na. 50/2017 ili kuipa nguvu TFRA kukokotoa, kutangaza
na kusimamia bei elekezi ya mbolea.
Aliwaagiza
pia wafanyabiashara wanaotunza mbolea bila kuzingatia viwango
vilivyowekwa na TFRA kuacha haraka tabia hiyo kwani kwani wanasababisha
mbolea kumfikia mkulima ikiwa imepungua ubora au kuharibika kabisa na
hivyo kumfanya mkulima asipate tija inayotokana na matumizi ya mbolea.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amewataka wataalamu hao Kutenda
haki katika uwajibikaji wao, Kufanya kazi kwa weledi, uaminifu,
uwajibikaji uliotukuka, na nidhamu ya hali ya juu.
Aliongeza
kuwa kwa yeyote atakaye kwenda kinyume na matakwa ya serikali ya awamu
ya tano inayoongozwa na Mhe rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Dkt John Pombe Magufuli itamchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria.
Post a Comment