Jana
tarehe 28 Agosti, 2017 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya za
Wanafunzi watanzania wanaosoma katika Jamhuri ya watu wa China (TASAFIC)
Bw. Remidius Mwema Emmmanuel alikutana na kufanya mazungumzo na Naibu
waziri wa Vijana, Kazi na Ajira Nchini Tanzania Mhe. Anthony Mavunde.
Mazungumzo
hayo yaliyofanyika Ofisini kwake mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine
yalilenga ufahamu juu ya nafasi ya vijana wa kitanzania wanaohitimu
masomo yao nje ya nchi hususani China namna ambavyo wanaweza kunufaika
na kutumia vema fursa mbalimbali za kiuchumi kwa manufaa ya Taifa pindi
wanaporejea nchini baada ya kuhitimu masomo yao. Hata hivyo Mhe.
Mavunde
alipokea maelezo mafupi juu ya mkakati wa Shirikisho (TASAFIC) kwa
Vijana wa Kitanzania pindi wanapohitimu wanavyoweza kuwa chachu ya
mabadiliko na kuchangamkia fursa zilizopo nchini kwa kutumia Uzoefu na
taaluma wanayoipata nje ya nchi. Kwa upande wake Mhe. Mavunde alipongeza
juhudi kubwa zinazofanywa na TASAFIC na kuongeza kuwa Serikali Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania iko tayari na inaendelea kuwaunga mkono Vijana
wote wanaoonyesha uthubutu wa kujikwamua kiuchumi.
Akizungumzia
Upande wa kilimo, alisema baadhi ya Vijana wamekuwa na mitizamo ya
kutojihusisha na Kilimo, Lakini hii inatokana na wengi wao kujaribu
kilimo kwa kutozingatia kanuni na misingi bora ya Kilimo na kuona jambo
hilo haliwezekani.
"Serikali
sasa tuna mikakati ambayo tuna hakika itasaidia kuondoa dhana hizo na
kuwafanya vijana wengi kupenda kilimo, ikiwa ni pamoja na Kutoa Elimu
zaidi na kuwatumia vijana waliofanikiwa ili waweze kuaelimisha wenzao.
Mfano tunao vijana wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA)
wanaitwa SUGECO, Serikali iliwapatia udhamini wa fedha kupitia Benki ya
CRDB, wakafanya kilimo na sasa wamekuwa ni taasisi kubwa na wameanza
kusaidia vijana wenzao kupitia mafunzo na misaada mbalimbali.
Lakini
wapo vijana Mkoani Mbeya, Ruvuma na Mikoa mingine ambao wamepata
mafanikio makubwa. Jambo la msingi ni vijana kubadili mitizamo, tunayo
Benki yetu ya maendeleo ya kilimo, Mifuko ya pembejeo, Mifuko ya
uwezeshwaji wananchi na mfuko wa maendeleo ya Vijana hiyo ni hatua
mojawapo lakini bado Serikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha vijana
kupitia vikundi rasmi wanajenga utayari wa kujihusisha na kilimo, hata
kilimo cha muda mfupi (Mboga mboga) ambacho pia kimeleta manufaa makubwa
kwa makundi ya Vijana.
Sasa
ni waombe mtambue kwamba nynyi TASAFIC kupitia watanzania wote
wanaosoma China Taifa linawategemea na ni matarajio yetu kwamba Taaluma
zenu zitatumika kikamilifu kubadilisha kundi kubwa la vijana pale
mtakaporejea nchini " Alisema Mhe .Mavunde Akitoa shukrani kwa Naibu
waziri huyo, Bw. Remidius kwa niaba ya TASAFIC amesema TASAFIC
Itaendelea kutumia Fikra,Taaluma,mawazo na kutoa maoni mbalimbali yenye
lengo la kuleta tija kwa Taifa.
“Mhe
.Naibu waziri nakuhakikishia kwamba TASAFIC itaendelea kuwajibika na
kuwatumikia watanzania wote wanaosoma Jamhuri ya watu wa China chini ya
ungalizi wa Ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini China na nitafikisha
ujumbe kwa wasomi hao,Ikiwa ni pamoja na kuielezea vyema na kuwakumbusha
fursa njema na mikakati ya Serikali iliyopo kwa wasomi hao pindi
watakapohitimu Masomo yao na kurejea nchini (Tanzania).
Ingawa
Miongoni mwa wahitimu kutoka Chuo Kikuu Cha Kilimo Nchini China kwa
mwaka 2017 baada ya kurejea nchini tayari wameonyesha nia kuanzisha
Shamba maalum la Mfano kulima zao la Muhogo, aidha Tunacho chama cha
Jumuiya ya Watanzania ambao waliowahi kusoma China (CAAT) ambao pia
wameendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha taaluma,Uzoefu na
Maarifa ya watanzania wote waliosoma China yanatumika kikamilifu kwa
manufaa ya Taifa,” Alisema Katibu Mkuu Remidius Emmanuel
Post a Comment