Serikaliya JPM ndiyo iliyochaguliwa na watanzania wengi na iko kikatiba, hivyoni halali. Hivyo serikaliya JPM siyo ya dikteta.Kumekuwepo madai kwamba JPM anawanyanyasa watanzania na hashauriki. Siyo kweli, JPM analo baraza la mawaziri linalomshauri na anacho chama chake kinachomshauri. Pia anao watalaam wanaomshauri katika masuala mbalimabali.Hivyo hola hizi hazina mashiko.
Kwa muda mfupi, serikaliya JPM imeonyesha mwelekeo wenye kuleta matumaini kwa mwatanzania.
• JPM ameonye sha dhamira ya kweli ya kupiga vita ufisadi ukilinganisha na baadhi ya vyama vinavyompigia kelele kwamba ni dikteta.
• JPM anapiga vita rushwa, uzembe kwenye serikali, ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka.
• JPM anachukua hatua kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha watanzaniawengi
• JPM anasimamia kwa karibu watendaji na kufuatilia kwa karibu kero za wanachi, hakuna ombwe la uongozi.
• JPM ameweza kuchua maamuzi magumu, mfano elimu bure; mchanga wa madini usipelekwe nje ya nchi.
• Hatua alizochukua JPM dhidi ya wizi bandarini na sehemu nyingine zinaonyesha uzalendo wake.
• JPM anatekeleza vizuri iIlani ya uchaguzi ya chama chake kilichopewa ridhaa kuongonza na watanzania.
Kwa hatua hizo alizochukua JPM ni mtanzania yupi mzalendo ambaye amenyanyaswa au kuonewa kwa hatua hizo ? Au kwa hatua hizi mtanzania yupi anagandamizwa ?
Kwa ujumla, JPM ameleta heshima kwa nchi yetu hadi nchi za nje zinaanza kuchukua hatua ambazo JPM amezichukua hapa Tanzania.
Mtanzania yoyote anayenung’unika kwa hatua hizi zilizochukuliwa naserikal ya JPM nidhahiri uzalendo wake unawalakini na nidhahiri pia anapigania maslahi yake binafsi au ya kukudi cha watu fulani wachache wala si maslahi mapana ya nchi yetu.
Lakini pamoja na hayo yote baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani tena wenye elimu nzuri wana mkejeli na kumwita JPM eti dikteta uchwara, KWELI INASIKITISHA.
Lakini, ni kwa lipi hasa wamwite dikteta uchwara?
Wapo wanachama wa chama kimoja wanawasifu hawa viongozi waliokamatwa na kuachiwa kwa dhamana eti ni mashujaa.
Je ni kipi cha maana na heshima kwa nchi yetu wanachokipigania hadi waitwe mashujaa?
Ushujaa wao ukowapi? Je kukamatwa na kuwe kwa rumande kwa kuitukana serikali ni ushujaa ?
Je kuwekwa rumande na baadae kupata dhamana kwa kuandamana bila kibali cha polisi ni ushujaa ?
Je kukamatwa na vyombo vya dola kwa kukaidi maelekezo ya vyombo hivyo ni ushujaa?Hapana. Kama kwenye mikutano au makongamano yanayofanyika nje ya Nchi wanawaita mashujaa ni mashujaa wao siyo mashujaa wetu.
Wanacho kifanya wanachama hawa ni upotoshaji wenye lengo la kuvuruga amani ya Nchi yetu. Watanzania tukatae upotoshaji huu na tuwapuuze. Nawasihi watanzania tuiunge mkono serikaliya JPM.
Juzi kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Democrati huko Marekani Mama Obama amewatahadharisha na kuwataka wamarekani kuwapuuza viongozi wanaotukana ovyo hadharani kwani wanajenga fikra mbaya kwa vijana wa marekani. Mama Obama alikuwa anamzungumzia mgombea wa chama cha rebublican ambaye nimsema ovyo, ambaye ana lugha ya matusi kwa viongozi na amekuwa akimtukana rais Obama kwenye mikutano. Mama Obama ameuliza, Je vijana wa marekani wanajifunza nini kwa viongozi hawa wanaotumia lugha chafu hadharani? Ni dhahiri maadili ya vijana wa marekani yatakuwa hatarini. Kwa mtazamo huo wa Mama Obama, vijana wetu hapa Tanzania wanajifunza nini wanaposikia lugha za matusi kutoka kwa viongozi wa vyama vya siasa ?.Vita ni siasa inayo mwaga damu kwani haina majadiliano wala ushawishi. Ni ugomvi.Vyama vya siasa viepukane na ugomvi. Vijenge hoja na viwashiwishi watanzania kuhusu sera zake.
Je ikitokea kijana akamwambia baba yake kwamba ni baba uchwara atajisikiaje?Au akakuambia wewe mama ni mama uchwara. Je utafurahi jirani yako akimpongeza huyo kijana na kumwita shujaa ?
Je haiwezekani kudai haki na demokrasia na kutoa maoni na kuikosoa serkali bila kutumia matusi na kejeli kwa serikali iliyoko madarakani?.Upinzani ujifunze kwamba, siasa za kiuanaharakati kwa Tanzania hazikubaliki. Tanzania iliisha pata Uhuru wake.
Tukumbuke Nyerere alidai uhuru kwa kutumia hoja za msingi hadi wakoloni wakatoa uhuru. Siasa ni vita isiyo mwaga damu. Ni majadiliano na ushawishi. Hata sasa inawezekana kudai haki, kutoa maoni na kuikosoa serikali bila kutumia lugha ya matusi.
Mtu yeyote asiyetaka kuongozwa hawezi kupata fursa ya kuogoza.
By Fred Mpendazoe
Post a Comment