PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) KUCHANGIA ZAIDI YA BILIONI 34 YA GAWIO LAKE KWA SERIKALI MWAKA HUU WA FEDHA 2016/2017
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Maliasilia na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka baina ya Hifadhi za Taifa,...
Waziri wa Maliasilia na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka baina ya Hifadhi za Taifa, Wahiri na Waandishi wa aandamizi wa habari nchini, ulioanza leo jijini Tanga.
 
 NA: ANDREA NGOBOLE PMT
Wahariri na Wanahabari nchini wametakiwa kuhakikisha wanaendelea kutumia vyema kalamu zao katika kuandika masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya  utalii wa Tanzania ili kuutangaza ikiwa sambamba na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe wakati akifungua mkutano wa sita wa wahariri na wanahabari waandamizi unaohusu sekta ya utalii nchini ambao umeandaliwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA) unaofanyika jijini Tanga mapema leo ukiwa na kauli mbiu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda.
Waziri Maghembe amesema sekta ya habari ina mchango mkubwa katika kukuza sekta ya utalii nchini, hivyo wanahabari wanatakiwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii kupitia habari na makala mbalimbali wanazoandika.
"Mchango wa vyombo vya habari ni muhimu sana katika kukuza sekta ya utalii, mmekuwa mnaandika sana lakini naomba muendelee kuandika zaidi ili tuweze kuwa na sekta ya utalii yenye ustawi mzuri," amesema.
 
Pia amewataka  wanahabari kuhakikisha wanaandika habari zenye tija kwa jamii kwani utalii umekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi na kwamba una changamoto kubwa kwani wanashindana na nchi nyingine zinazotegemea utalii kama Kenya,Uganda, Rwanda, Msumbiji na Afrika kusini
  "Nyinyi waandishi wa habari msikubali kuandika jambo ambalo hamlijui kitaaluma, kwani ukifanya hivyo utakuwa hujengi jamii yako,hivyo ni muhimu sana kwa wanahabari kujua habari sahihi za uhifadhi hasa kwa kuzungumza na wataalamu kutoka sekta hiyo"amesema Prof. Maghembe. Amesema kwa sasa watu mbalimbali duniani wanafahamu kuhusu vivutio vilivyopo nchini na hiyo ni kutokana na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi amesema wataendelea kushirikiana na vyombo vya habari ili kuhakikisha watanzania na watu mbalimbali duniani wanavifahamu vizuri vivutio vyvutalii vya Tanzania
  amesema kuwa utalii Utalii unachangia 17.2% ya pato la Taifa na 25% ya fedha za kigeni nchini,80% ya utalii unatokana na Hifadhi za Taifa.

Amesema kuwa TANAPA inajitegemea kwa asilimia 100, na mchango wao kwa serikali umeongezeka kutoka bilioni 27 mwaka 2015/16 mpaka bilioni 34 kwa mwaka 2016/17 sawa na ongezeko la bilioni saba.

"Tanzania ina vivutio vingi vya kipekee ukilinganisha na nchi nyingine Duniani,Mamlaka kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii nchini pamoja na Ofisi za Balozi zetu nchi mbalimbali inajitangaza ndani na nje ya Nchi ili kuongeza idadi ya Watalii",amesema Kijazi.

Akielezea Uvumi wa Mlima Kilimanjaro kuwa haupo Tanzania,anasema ni ni propaganda za ushindani wa kibiashara, lakini matumizi ya Teknolojia yamesaidia kutoa elimu,anasema na kuongeza kuwa hivi sasa idadi kubwa ya watalii kutoka Nje ya nchi wanaelewa Mlima huo upo Tanzania.

Akielezea changamoto ya Ujangili,Kijazi anaeleza kuwa kwa sasa matukio ya ujangili yamepungua kwa 80% na kwamba Mamlaka inashirikiana na Jumuia ya Kimataifa kutokomeza Soko la bidhaa zinazotokana na ujangili.

Kijazi alimaliza kwa kusema kuwa TANAPA ilianzishwa kisheria mwaka 1959 kukiwa na hifadhi moja tu ya Serengeti,lakini mpaka sasa hifadhi zimeendelea kuongezeka hadi kufikia 16 mwaka 20
Meneja mahusiano wa shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) Pasco Shelutete akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo hii leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi akizngumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Tanga leo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela akizungumza wakati wa mkutano
Washiriki wa mkutano hao wakifuatilia hotuba za ufunguzi zilizokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani, Dk James Wakibara akiwasilisha mada ya changamoto za mifugo katika hifadhi za taifa katika mkutano huo.
Maofisa wa TANAPA wakifuatilia mada

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo.
Picha ya pamoja baina ya washiriki na mgeni Rasmi.
 

 
Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe akizungumza jambo alipokuwa akifungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia yaliyaokuwa yakijiri kwenye mkutano huo ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Allan Kijazi akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe kufungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh Martin Shigella akiwakaribisha wageni mbalimbali waliofika kuhudhuria mkutano wa mwaka wa Wahariri na Wanahabari waandamizi,uliofanyika kwenye ukumbi uliopo kwenye ofisi zake.Mkutano huo umebeba kauli kuu ambayo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Allan Kijazi akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe kufungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Baadhi ya Wahariri wakifuatailia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga
Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,ambapo kauli mbiu kuu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd.Absalom Kibanda akitoa salamu za shukurani kwa waandaji wa mkutano pia na kueleza changamoto kadhaa zinazopaswa kurekebishwa/kufanyiwa kazi na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Baadhi ya Wahariri wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
 
 
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top