Na Tiganya Vincent, NZEGA
Madiwani
katika Halmashauri za Mkoa wa Tabora wametakiwa kuepuka kujenga
makundi miongoni mwao ambayo yamekuwa yakisababisha wananchi
waliowachagua kuchelewa kupata maendeleo kwa sababu ya muda mwingi
kushughulikia migogoro badala ya kutatua matatizo mbalimbali ya
wananchi.
Hayo
yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati akifunga
mafunzo ya siku nne ya Madiwani na Watendaji wa Manispaa ya Tabora
yaliyofanyika wilayani Nzega kuhusu jitihada za jamii kupitia mbinu
shirikishi jamii ya fursa na vikwazo kwa maendeleo (O&OD)
iliyoboreshwa na usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo (LGDG)
Alisema
makundi yatawafanya washindwe kuwajibika vizuri na kujikuta miaka
mitano ya uongozi wao inakwisha bila kuwafanyia chochote wananachi zaidi
ya kupigania kuondoana katika uongozi badala kukazania maslahi ya
wananchi.
“Nyie
ndio mliko zamu sasa mkiendekeza makundi na migogoro isiyokwisha,
mtajikuta zamu zenu zinamalizika hamjawafanyia chochote wananchi
waliowachagua badala yake kupambana kila mnapokutana katika vikao vyenu
….kila kikao itakuwa sisi hatumutaki fulani atuongoze au fulani fulani
hatufai” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Bw.
Mwanri aliongeza kuwa wakimruhusu Shetani wa namna hiyo apite kati yao
hakuna tena kazi wala maendeleo kwa wananchi wao waliowachagua.
Alisisitiza
kuwa viongozi wa aina hiyo wanakuwa wamekosa sifa ya kuendelea
kuaminiwa na jamiii iliyowachagua tena kuwatetea wananchi katika
matatizo yanayokwamisha maendeleo yao.
Mkuu
huyo wa Mkoa aliwataka Madiwani wote washirikiane bila kujali itikadi
za vyama vyao, dini zao, kabila zao katika kuhakikisha kuwa wanatetea
vyema wananchi wao na wanasimamia vyema watendaji wa Halmashauri zao kwa
ajili ya kuwaletea wananchi maisha bora.
Naye
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Leopold Chundu Ulaya alisema kuwa
mafunzo walipatiwa na wawezeshaji kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa
Hombolo na TAMISEMI yatawasaidia kuhakikisha kuwa miradi yote inatekezwa
kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.
Alisema
kuwa watajitahidi kuunganisha nguvu kwa pamoja kwa kubadilika ili
kuhakikisha kuwa wanatatua matatizo ya wananchi waliowachagua na
kuwaletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Post a Comment