MWIGULU Nchemba Atoa ONYO Kali Kwa Wanaompinga Rais Sakata la Wanafunzi Kupewa Mimba
Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumapili wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Parokia ya Kisasa Mjini hapa.
Amesema Serikali haitaomba ushauri wala maoni kwa sababu maelezo yaliyotolewa na Rais, John Magufuli ni maagizo ya Serikali.
Waziri huyo amesema Serikali imetoa haki ya kila mtoto kupata elimu kwa kuifanya kuwa bure kwa hiyo atakayeikosa asitafute kisingizio.
"Rais ametoa haki hiyo sasa hivi elimu ni bure, halipi tuition wala nini, atakayeamua kuachana na haki hiyo asitafute kisingizio, asipeleke lawama kwa Serikali, "amesema.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.