WILLIAM Lukuvi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesababisha mtafaruku kwa muda mfupi baada ya kutinga kanisani na ving’ora vya jeshi la polisi, anaandika Dany Tibason.
Mtafaruku huo umetokea leo alipokuwa amesindikizwa na gari mbili za jeshi la polisi huku gari hizo zikiwa na mwendo kasi na vingora jambo ambalo liliwafanya wananchi waliokuwa katika ibada ya kuaga mwili wa marehemu Philimon Ndesamburo kushtuka.
Magari ya polisi yenye namba za usajili PT 1971 na PT 1936 yalikuwa yakimsindikiza Lukuvi huku ving’ora vikilizwa kana kwamba kuna tukio kubwa jambo ambalo liliwafanya waumini katika ibada hiyo kuwa na wasiwasi juu ya ujio wa magari hayo ya polisi.
Mmary Mallya, Mmoja wa waumini amesema serikali imekuwa na tabia ya kutumia vibaya mamlaka yao ikiwa ni pamoja na kuwatumia jeshi la polisi kuvuruga amani ya nchi kwakuwa kitendo hicho kimetafsiriwa kama ni kitendo cha kutaka kuvuruga amani ya ibada hiyo na kuhoji ni kwanini Waziri Mstaafu wa awamu ya tatu Fredrick Sumaye na Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne Edward Lowassa kuingia bila kuwa na ving’ora vya polisi.
“Tumekuwa na msiba huu mzito lakini hatujaona viongozi wa serikali wafanye jambo lolote imefikia hatua ya serikali kuzuia uwanja Mashujaa kwa ajili ya kumwaga marehemu, hapa wamekuja viongozi mbalimbali wa chama pamoja na viongozi wakuu wa serikali ambao wapo chadema lakini hawakuja na ving’ora.
“Hapa tunajuiliza huyu Lukuvi kuja na magari mawili ya jeshi la polisi huku yakiwa yameshehena askari wenye siraha za moto maana yake nini, tena anakuja na ulinzi mkali kanisani si bora asingekuja badala ya kufanya mambo ya kuwatishia wananchi ambao wamemiminika ibadani” amesema Mally.
Naye Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini amesema kitendo cha serikali kuendelea kuwatishia wananchi katika maeneo mbalimbali ipo siku ambapo uvumilivu utakwisha na wananchi watadai haki zao kwa nguvu.
Amesema kuwa isifike hatua serikali ikaona busara ya upinzani ni ujinga na wala ujinga siyo kuwa busara lakini hali inavyoendelea hasa katika kuvuruga amani ya Arusha na sehemu nyingini utawala unatakiwa kujia kuwa kwa sasa dunia ni sawa na kiganja.
Lema alisema kuwa inasikitisha kuona kwa muda mfupi ambao mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kukaimu mkoa wa Kilimanjaro tayari ameonesha kuwachanganya wananchi na kuwakwaza kwa kiasi kikubwa jambo ambalo Lema amesema linawatia wananchi hasira.
Post a Comment