Diwani wa kata ya Murieti jijini Arusha Kredo Kifukwe alipokuwa akitangaza kuachia ngazi ya udiwani na kujiondoa rasmi chadema mbele ya wanahabari mapema leo |
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Diwani wa
kata ya Murriet kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Kredo Kifukwe ametangaza kujiuzulu rasmi
katika Nafasi ya Udiwani wa kata hiyo iliyoko Wilaya ya Arusha mkoani Arusha .
Kredo
ameeleza kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo ili aweze kutumikia jamii kama raia
mwema bila kuegemea upande wowote kisiasa
lakini pia amesema kuwa juhudi zinazofanywa na Raisi John Pombe Magufuli
zimemfanya ajiuzulu kwani haoni sababu ya kuendelea kumpinga kutokana na kazi
nzuri anayoifanya ya kulitumikia taifa bila kujali itikadi za kisiasa.
Diwani huyo
aliyejiuzulu amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kujiunga na chama chochote
cha siasa kwani ataendelea kuwa raia mwema na kuitumikia jamii yake pamoja na
taifa huku akiendelea kuunga mkono juhudi za Rais.
Kaimu
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Injinia Gaston Pascal amethibitisha kupokea
taarifa za kujiuzulu kwa diwani huyo ambaye aliwasilisha barua ya kujiuzulu
katika Ofisi za Mkurugenzi kwa mujibu wa sheria hivyo watafikisha taarifa kwa
tume ya uchaguzi ili uchaguzi uweze kufanyika kuziba pengo hilo.
Post a Comment