ASKOFU mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi
ya Iringa, Blaston Gaville, amemuomba Rais Dk. John Magufuli kumalizia
mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya ulioachwa na mtangulizi wake.
Akizungumza baada ya kuwekwa wakfu Askofu Gaville na msaidizi wake,
Himidi Sagga, katika ibada iliyofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya
Msingi, Gangilonga, alisema Wakristo na Watanzania kwa ujumla wana
imani kubwa na Serikali ya Dk. Magufuli na ni matarajio yao kwamba
mchakato wa kuandika Katiba mpya utamalizwa kama lengo lilivyokuwa.
Askofu huyo alisema Dayosisi ya Iringa inatoa mwaliko kwa vyama vyote
vya siasa na jamii nzima ya Watanzania kuendeleza kukuza tunu ya
ushirikiano na moyo wa kizalendo ili kuwa na maendeleo yenye tija kwa
wananchi na Taifa kwa ujumla.
Katika ibada hiyo, Askofu Gaville alieleza kuwa wanatiwa moyo na
jitihada zinazoendelea kufanywa na Dk. Magufuli katika kufufua uchumi na
kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania
wote na
kwa kufanya hivyo, ni faraja kubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
“Kweli nasema nchi yetu ina wanyonge wengi kuliko wenye nguvu, tunatiwa
moyo na rais na Serikali yake tunapoona wanatetea wanyonge,” alisema
Askofu Gaville.
Hata hivyo, askofu huyo aliiomba Serikali iangalie upya suala la kodi
kwa mashirika ya dini kwakuwa baadhi ya kodi wanazolipa ni kwa
kuendeleza elimu kupitia vyuo vya ufundi.
“Katika kuunga mkono jitihada za Serikali, kanisa linasaidia watoto
masikini wapate haki yao ya elimu, tunaomba Serikali isituingize katika
kundi la watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo kwa sababu wanasoma
shule binafsi.
Chanzo: Mtanzania
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment