PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MRISHO GAMBO AZINDUA MRADI WA MAJI ULIOGHARIMU MILIONI MIA MBILI WILAYANI NGORONGORO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa mkoa Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amezindua mradi mkubwa wa maji wa maji kwaajili ya kunyweshea mifugo(cattle trough) na matum...


Mkuu wa mkoa Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amezindua mradi mkubwa wa maji wa maji kwaajili ya kunyweshea mifugo(cattle trough) na matumizi ya binadamu katika kata ya Ndepes wilayani Ngorongoro.
 
Mradi huo mkubwa wa maji umetumia takribani milioni 200 ikiwa ni gharama nzima za mradi huo, utekelezaji wa mradi huo umesimamiwa na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni utekelezaji wa agizo la waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alilolitoa mapema mwezi wa Desemba 2016, moja ya maagizo yake ilikua ni wananchi kujengewa mfumo wa maji kwa matumizi yao na mifugo yao ili kuzuia  uingizwaji wa mifugo katika crater ya Ngorongoro.
 
Aidha Mhe. Gambo ameipongeza mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kuutekeleza mradi huo kwa wakati na kuendelea kutoa msisitizo kwa wananchi kuwa agizo la kutoingiza mifugo ndani ya crater linaendelea na amezitaka mamlaka kuanza mchakato wa kuligeuza agizo hilo kuwa sheria ili liweze kutekelezeka kwa vitendo zaidi.
 
Wananchi wa eneo la Ndepes wameishukuru sana serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza ahadi yake ya kuhakikisha wananchi hawafuati maji umbali zaidi ya mita mia nne kama ilivyo ahidiwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
 
mkuu wa mkoa wa Arusha akizindua mradi huu wa maji






Mrisho Gambo akimtwisha dumu la maji mmama wakati wa uzinduzi wa mradi huu wa maji uliogharimu milioni mia mbili

mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na wananchi wa Ngorongoro wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa maji
mifugo ikinywa maji katika lambo lililopo kijijini hapo Ikiwa ni sehemu ya mradi huo

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top