wanafunzi wa kike nao hawakuwa nyuma katika kupanda miti shuleni hapo |
wanafunzi wa shule ya sekondari Benjamini Mkapa wakipanda miti siku ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti mererani |
wanafunzi hao wakipanda miti katika eneo la shule yao huku wakisimamiwa na mwalimu wao |
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera
amezindua kampeni ya upandaji miti katika mji wa Mererani,wilaya ya Simanjiro
huku akitoa wito wananchi mkoa wa Manyara kuzitumia mvua zinazonyesha kupanda
miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza katika uzinduzi huo juzi, ambao umeanzishwa na
kampuni ya Tanzanite One, katika shule ya Sekondari, Benjamin Mkapa,Dk Bendera
alisema,mji huo ambao kwa kawaida hauna mvua za kutosha unapaswa kutumia mvua zinazoendelea kupanda miti.
“kila kaya lazima ipande miti sasa,ili kuondoa hili jangwa
na kutokana na mvua hizi tunauhakika miti mingi inakuwa na kubadilisha kabisa
mazingira ya Mererani”alisema
Akizungumzia mradi huo, Mkurugenzi wa Tanzanite One, Hussein
Gonga alisema,kampuni hiyo, imejipanga kuondoa tatizo la ukame Mererani, kwa
kuanzisha kampeni ya kupanda miti 1000 awamu ya kwanza.
Gonga alisema kampuni
hiyo, imetenga kiasi cha sh 4milioni, kwa wanafunzi wa shule ya Benjamin Mkapa
ambao watafanikisha mradi huo, kwa njia ya kushindana madarasa manne, kidato
cha kwanza hadi cha nne.
“darasa ambalo miti yake, itakuwa vizuri litapata zawadi y
ash 2.5 milioni, washindi wa pili 1 milioni na washindi wa tatu 500,000 lengo
ni kuhakikisha miti yote 1000 inakuwa”alisema
Alisema dunia hivi sasa inakabiliwa na tatizo kubwa la
mabadiliko ya tabia nchi,maeneo mengi kuna ukame,wanyama na binaadamu hawana
mvua na maji hivyo, njia pekee ya kujikomboa ni kupanda miti.
Kwa upande wake,Mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Faisal
Shabhai alisema,baada ya kampeni hiyo, kufanikiwa katika shule ya Benjamin
Mkapa,watahakikisha inahamia katika shule nyingine za Mererani na katika
vikundi vya utunzwaji wa mazingira.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Benjamin Mkapa, Emmanuel
Kato,alisema mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la ukame Mererani naa pia
kuboresha mazingira ya shule na Mererani kwa ujumla.
“tunaishukuru kampuni ya Tanzanite One kwa kuleta hapa
shuleni kwetu mradi huu na pia wameahidi kutujengea uzio wa kuzunguka shule na
kuboresha kisima kirefu cha maji ambacho
walituchimbia illi tupate maji ya kutosha”alisema
Mwanafunzi wa shule hiyo, Aisha Abdi alisema, wamejipanga
kila darasa kuhakikisha wanashinda
zawadi kwa kuitunza vyema miti
waliyopanda ambayo pia itasaidia kuboresha hali ya hewa katika shule hiyo.
Post a Comment