PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: ALICHOSEMA Zitto Kabwe Baada ya Adam Malima Kuonyeshwa Bunduki na Polisi Jana..!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Mbunge wa Kigoma Mjini, Zuberi Zitto Kabwe amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na moja ya askari polisi kumtis...



Mbunge wa Kigoma Mjini, Zuberi Zitto Kabwe amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na moja ya askari polisi kumtishia bunduki aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima.

Zitto kabwe ameonyesha masikitiko hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook akihoji kama polisi wanafundishwa kuwafanyia hivyo raia.

"Hii ni nini ?, askari wetu wanafundishwa kufanya hivi, Waziri Mwigulu huyu yupo wazi na ni wa kutoka kwako. Unahitaji uchunguzi". Ameandika Zitto 

Zitto ameandika hayo baada ya masaa machache kupita kwa tukio hilo lililowahusisha askari hao walioambatana na kampuni ya Majembe Auction Mart waliokuwa wakitaka kujaribu kukamata gari iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara ya Masaki karibu na Hoteli ya Double tree ingawa ndani ya gari hilo alikuwepo dereva.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top