NA: ANDREA NGOBOLE PMT
Wananchi
wa jamii ya wafugaji wanaoishi katika kata ya Naisinyai wilaya ya
Simanjiro inayopakana na machimbo ya Tanzanite wameshauriwa kuanza
kujikita katika ujasiriamali badala ya kutegemea mifugo pekee.
Mkurugenzi
mwenza wa kampuni Tanzanite One,Faisal Juma alitoa wito huo jana wakati
akitoa msaada wa sh 15 million kwa wanawake wa Kata hiyo ili kuanzisha
chama cha kuweka na kukopa(SACCOs).
Juma
alisema, wananchi wa Naisinyai wamepata fursa ya kuwa katika eneo
ambalo yanachimbwa madini ya Tanzanite hivyo ni muhimu wanufaike nayo
kwa kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali na kufanyabiashara
,kuchimba na kuuza madini hayo.
"Sisi
kama Tanzanite One tunawajibu kuwasaidia kuwa wajasiriamali kwani
tunachimba madini katika kata yenu na huu ni msaada kwa wajasiriamali
lakini bado tutaendelea kusomesha watoto wa Kaya masikini na kutoa
Michango mingine"alisema
Alisema
mabadiliko ya tabia nchi yameathiri sana mifugo hivyo ili kutoathiri
maisha ya wafugaji wanapaswa kuwa na mbadala wa kidogo wa kuwasaidia
kimaisha.
Awali
mwenyekiti wa kijiji cha Naisinyai,Taiko Laizer alishukuru michango
wawekezaji na kuwataka kupanua wigo wa kutoa ajira kwa wananchi wa
Naisinyai hasa wanawake.
'Tunajua mmewapa ajira vijana wa hapa lakini tunaomba zinapotokea ajira hasa wanawake tuongezewe"alisema
Naye Diwani wa viti maalum Kata ya Naisinyai Paulina Masekeni aliahidi fedha waliopatiwa
Wanawake wa kata hiyo zitatumika kuanzisha vikundi vya ujasiriamali kama walivyo omba.
Post a Comment