Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima amesema kuwa
yeye ni sababu kubwa ya kutenguliwa kwa Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa
na Michezo Nape Nnauye.
Akizungumza leo (Alhamisi) baada ya kutembelea Ofisi za kituo cha redio
cha Efm,Gwajima amesema Mkuu wa Mkoa alivamia ofisi za Clouds kwa lengo
la kutaka wamchafue Askofu huyo lakini baada ya Nape kuunda tume
iliyofanya uchunguzi kumesababisha kutenguliwa kwake.
"Labda niseme kuwa sababu za Nape kutenguliwa zinanihusu sana mimi.Cha
kujiuliza ni kwamba ni nani alikuwa nyuma ya Mkuu wa Mkoa alipovamia
Clouds hadi Nape atenguliwe?”alihoji.
Gwajima alifika Ofisini hapo saa 4:06 na kukutana na viongozi na
wafanyakazi huku akiwapa pole na kuwatia moyo na kwamba watayashinda
majaribu yanayoikumba tasnia ya habari.
Post a Comment