PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Mbowe Apekuliwa Usiku......Arudishwa Polisi
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Jana  mchana Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alihojiwa na Polisi kuhusu sakata la dawa za kul...
Jana  mchana Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alihojiwa na Polisi kuhusu sakata la dawa za kulevya baada ya jina lake kutajwa kwenye orodha ya Makonda  February 8.

Baada ya kukaa kituoni hapo kwa zaidi ya masaa mawili Waandishi wa habari waliokua nje ya eneo hilo walishuhudia Mwenyekiti huyo akichukuliwa na Gari aina ya Land Cruiser iliyofatwa na magari mengine nyuma yake na kuelekea ambako Waandishi hawakufahamu mara moja.

Baadaye msemaji  wa CHADEMA Tumaini Makene alisema  Polisi walienda na Mbowe kupekua nyumba zake na kuandikisha maelezo ya majirani ambapo alisema kwenye mida ya saa sita usiku wa kuamkia leo Polisi walimrudisha Mbowe kwenye kituo cha Polisi kati na wakamfungulia jalada la Uchunguzi….

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top