Mhe,Jaji Mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatuma Hamis Masengi |
Picha ya pamoja kati ya waheshimiwa majaji kanda ya Arusha na Kilimanjaro ,Wakwanza kulia ni mhe,Jaji Dkt.Modesta Opiyo,Wakwanza kushosto ni mhe,Jaji Salma Maghimbi,akifuatiwa na aliyeko kushoto kwake mhe,Jaji Sekela Mushi,akifuatiwa na mhe,Jaji mstaafu Fatuma Hamis Masengi wakiwa na majaji wengine pamoja na waheshimiwa mahakamu.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mhe,Jaji Mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatuma Hamis Masengi akiwa na waheshimiwa mahakimu wa mahakama ya mwanzo(waheshimiwa mahakimu hao wamelelewa na mhe,Fatuma Masengi)
Picha ya pamoja ya waheshimiwa majaji pamoja na mawakili wa serikali,na wale wa kujitegemea.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus.
Sherehe za kumuaga aliyekuwa Jaji mfawidhi wa mahakam kuu kanda ya Arusha Mhe,Fatuma Hamis Masengi ,zimefanyika leo katika mahakama kuu ya ndanda hiyo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo majaji,mahakimu,mawakili wasajili wa mahama watendaji pamoja na wageni waalikwa.
Sherehe
hizo zimeanza majira ya saa asubuhi katika mahakama ya wazi
ambapo Jaji Fatuma alianza kufanya kazi mnamo mwaka 1974 katika
mahakama ya mwanzo na
kuendelea kuitumikia mahakama hadi alipoteuliwa kuwa jaji mfawidhi
mahakama kuu.
Amewataka
majaji na mahakimu pamoja na wale wote wanaofanya kazi za kimahakama
wafanye kazi kwa kumtegemea Mungu huku wakijua kazi yeyote ina
changamoto zake hivyo ni vyema kufanya kazi kwa weledi zaidi na kwa
kuzingatia sheria inavyosema,wakimtendea haki kila mtu kwa stahiki.
Amewataka
wanawake kutokukata tamaa huku akisema kuwa wanawake wanaweza kuliko
wanaume japo kuwa wakati mwingine wanaume wanaona kama vile wanawake ni
wanyonge lakini mwanamke anaweza pale ambapo anasimama kwa nafasi yake
na kulitumikia kusudi kwa wakati na weledi.
"Wanawake
wenzangu msikate tamaa na kujiona wewe ni dhaifu ,tunaweza msibweteke
unapopata nafasi itumie vizuri bila kuaharibu taratibu zilizowekwa
,fanya kazi kwa bidii na jamii itaona juhudi zako ,wanawake tunaweza
"alisema masengi.
Aidha
Jaji Fatuma amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kumuwezesha
kwa wakati wote ambapo amekuwa akifanya kazi yenye
majukumu mazito, amezishukuru Asasi za kiserikali na zile
zisizo za kiserikali,amewashukuru wale wote walioshirikiana nae katika
kipindi chote alichokuwa akitimiza majukumu yake ya
kikazi.
Post a Comment