PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: UVCCM LONGIDO YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA NA KWALIPIA BIMA ZA AFYA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
picha ya pamoja UVCCM wilaya ya Longido wakiwa katika kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation . Picha na Ferdinand Shayo ...
picha ya pamoja UVCCM wilaya ya Longido wakiwa katika kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation .Picha na Ferdinand Shayo

Baadhi ya Wajumbe  wa UVCCM wilaya ya Longido wakiwa katika kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation .Picha na Ferdinand Shayo


Kushoto ni Katibu  wa UVCCM wilaya ya Longido Isaya Karakara, Katibu Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel  na Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation  Joyce Kabati .Picha na Ferdinand Shayo

Kushoto ni Katibu  wa UVCCM wilaya ya Longido Isaya Karakara, Katibu Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel  na Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation  Joyce Kabati .Picha na Ferdinand Shayo

picha ya pamoja UVCCM wilaya ya Longido wakiwa katika kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation .Picha na Ferdinand Shayo


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Longido umetembelea kituo cha Watoto yatima na Wanaoishi katika mazingira magumu cha Masai Foundation kilichopo mji mdogo wa Namanga na kutoa msaada wa vyakula pamoja na vifaa mbalimbali.

Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko Amesema kuwa wameamua kushirikiana na jamii katika kusaidia watoto ikiwa ni moja kati ya michango wanayoitoa ili kutosheleza mahitaji muhimu yanayohitajika katika kituo hicho.

Robert Amesema kuwa jukumu la kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni la kila mwanajamii hivyo jamii inapaswa kujitoa kusaidia watoto hao.

Katibu Hamasa wa CCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel amesema kuwa vijana hao wameamua kujitoa kutoa msaada kwa jamii ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hivyo ameiomba jamii kujitokeza kwa wingi kuwasaidia watoto hao.

“Hawa ni watoto wetu sote kila mtu anapaswa kuona kuwa ana jukumu la kuwasaidia hawa watoto ili waweze kufanikisha ndoto zao”  Neema

Katibu  wa UVCCM wilaya ya Londigo Isaya Karakara na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya Tulli Lemanga aliyejitolea kuwakatia bima ya afya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wamesema  kuwa vijana hao wataendelea na utamaduni huo mara kwa mara katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto za watoto.

Mmiliki wa kituo hicho Joyce Kabati amewashukuru vijana hao kwa kutembelea watoto hao jambo ambalo linaleta faraja kwa watoto hao ambao na wanamahitaji mbalimbali ambayo yamewasilishwa na vijana hao.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top