PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: DIWANI Asiyejua Kusoma na Kuandika Aibuka Tena...Adai Anajua Kusoma
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Zikiwa zimepita wiki chache tangu diwani wa Boma katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Julist Kisoma asimamishwe kufan...



Zikiwa zimepita wiki chache tangu diwani wa Boma katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Julist Kisoma asimamishwe kufanya shughuli za udiwani akidaiwa kutojua kusoma, amefunguka akisema alisoma hadi darasa la saba lakini hakufanya mtihani wa mwisho.

Kisoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Mafinga, amesema anafahamu kusoma na kwamba, tuhuma dhidi yake zimetokana na msimamo wake wa kusimamia rasilimali za kata yake na halmashauri.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Charles Mkoga alitangaza kumsimamisha diwani huyo wa Chadema kufanya shughuli za udiwani ikiwamo kuhudhuria vikao hadi suala lake litakapopatiwa ufumbuzi na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.


Kwa taarifa yako inadaiwa kuwa halmashauri ya mji wa Mafinga ndio inayoingiza mapato makubwa sana kuliko Halmashauri yoyote nchini Tanzania ukiondoa manispaa ya temeke  kwa sasa na hii ni  kutokana na uuzaji wa mazao ya misitu inayolisha ukanda mzima wa Afrika mashariki.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top