PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: JESHI la Polisi Lafanya Ukaguzi Ofisi za Jamii Forums na Nyumbani kwa Mmiliki wa Tovuti Hiyo Maxence Melo
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Leo Jeshi la Polisi limefanya ukaguzi na mahojiano kwenye Ofisi za Jamii Media(Fikrapevu.com na JamiiForums.com) na walie...



Leo Jeshi la Polisi limefanya ukaguzi na mahojiano kwenye Ofisi za Jamii Media(Fikrapevu.com na JamiiForums.com) na walienda pia nyumbani kwa Mwanzilishi, Maxence Melo

Polisi walichoondoka nacho ni nyaraka za usajili wa Jamii Media ikiwemo Cheti cha Mlipa Kodi, Cheti cha BRELA na Leseni ya Biashara.

Tunaomba umma utambue kwamba Jamii Media haina servers wala min-server ofisini kwake, nchini Tanzania wala Afrika. Pili, tunaomba watumiaji wa JamiiForums.com wasitiwe wasiwasi juu ya usalama wa taarifa zao.
Teknolojia tunayoitumia (encryption) kumsajili mtumiaji wa JamiiForums.com haituwezeshi kumfahamu mtumiaji yeyote labda yeye akubali kwa hiari yake kujiweka wazi mtandaoni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top