PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Diamond: Dalali Alishangaa Watu Wengi Kuulizia Nyumba Niliyonunua SA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Diamond amedai kuwa idadi kubwa ya watu, hususan kutoka Tanzania ilikuwa ikipiga simu kwa wakala aliyekuwa akihusika na ...


Diamond amedai kuwa idadi kubwa ya watu, hususan kutoka Tanzania ilikuwa ikipiga simu kwa wakala aliyekuwa akihusika na mauzo ya nyumba aliyonunua Afrika Kusini kutaka kujua kama ameinunua kweli nyumba hiyo au alipiga changa la macho.

Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, Jumamosi iliyopita, Diamond alisema wengi walikuwa wakiiuliza nyumba hiyo kinafiki
hadi wakala alishangaa imekuwaje! “Baada ya yale maneno maneno, hata yule agent alishangaa ‘hii nyumba mbona sasa hivi inauliziwa’ maake ile wikiendi iliulizwa sana sababu birthday ya Zari ilikuwa Ijumaa so wikiendi kuanzia Jumamosi, Jumapili watu wakawa wanaenda eti kujaribu kutrack ‘vipi nyumba inapatikana.’

Kwahiyo baada ya hivyo wenye nyumba hata wakashangaa ikabidi Zari akawaambia kwamba mpenzi wangu ni celeb na ndio maana alivyopost watu wanaulizia kinafiki,” alieleza. “So baada ya hapo basi ikawa easy wakaitoa kwenye mtandao kabisa, halafu wakaweka kibango kwamba ‘sold out’ wamesahau tu chini kuandika Nasib Juma,” aliongeza Diamond.

Kwa upande mwingine staa huyo amedai kuwa aliinunua nyumba hiyo wa fedha alizozilipa mara moja ambazo ni takriban shilingi milioni 394 pamoja na fedha za transfer zaidi ya milioni 20. Diamond anadai hatua inayofuata ni kwenda kuipamba kwa kumtumia mtu wake wa decor. “Nataka kwanza nikapatengeneze, hapo sasa nataka kufanya ushembenduzi, watu wanafikiri nimefanya, kumbe bado sijafanya sababu vitu kama hivyo lazima uwe proud kwasababu mimi nimekuwa katika mazingira magumu sana kutoka Tandale,” alisisitiza.

“Kwahiyo ile kwangu mimi ni achievement kubwa, kumiliki nyumba South Africa sio kitu kidogo, na ndio maana nataka nikapapambe vizuri nikapitie njonjo haswaa halafu nikiingia South Africa ni mashauzi mengi sana. Of course sometimes you need to do that sababu unafanya kazi kwa bidii.”

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top