PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: UNAWEZA KUYAREPEA MAISHA YAKO KWA KUTUMIA MUDA WA ZIADA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Na Ferdinand Shayo,Arusha. Katika maisha ya kila siku tunakutana na changamoto nyingi,misukosuko mingi   ambayo wakati mw...

 Profile photo
Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Katika maisha ya kila siku tunakutana na changamoto nyingi,misukosuko mingi  ambayo wakati mwingine inatukatisha tama na kutupunguzia spidi ya mafanikio.

Ni ukweli usipingika kuwa tunahitaji muda wa ziada wa kujirepea mithili ya gari  lililotembea umbali mrefu na kupita katika makorongo,milima,mabonde na changarawe.

Baada ya mapito yote hayo unahitaji kufanyiwa matengenezo na maboresho ili uwe imara tena uweze kuhimili mitikisiko ya safari ya maisha.

Kujirepea ni muhimu ili uweze kurudi kati hali yako nzuri itakayokuwezesha kufanya vizuri katika maisha.

Bila kujirepea ni vigumu kupata nguvu ya kutosha kukabiliana na magumu katika maisha na kuyashinda  lasivyo hali itakua ngumu unaweza kufa moyo ama kuishia njiani katika safari yako ya mafanikio ya kibiashara,kielimu,kifamilia na kiuchumi.

Mambo Magumu tunayoyapitia duniani hayatuachi tulivyo yanaondoka na kitu cha thamani ndani yako haijalishi ni kikubwa au kidogo hivyo unahitaji muda wa kurejesha thamani iliyopotea ndani yako.

Ni muhimu kutenga muda wa kujifariji mwenyewe,kufarijiwa na kufarijiana ,kutiana moyo ili tuweze kusonga mbele katika safari ya maisha na kufanikiwa.

Ni vyema kujisomea vitabu vitakavyojenga mtazamo chanya ndani yako ,matumaini mapya,tazama video na kusikiliza sauti ambazo ni chanya zitakazokupa hamasa ya kutimiza malengo yako.
Unahitaji kukaa mazingira tulivu yenye ukimya ,mazingira yanayoponya  (healing inviroment) unashauriwa iwe ni mbali kidogo namazingira ya  nyumbani ambayo umeyazoea ,mazingira yenye kijani ,uoto wa asili,maji,chem chem kwa kutazama maji pia unaweza kupunguza msongo wa mawazo.

Pata Muda wa kujisikiliza ,kusikiliza sauti iliyoko ndani yako inayokukumbusha juu ya kusudi la maisha yako duniani kwamba uko duniani kwa kazi maalumu hauko duniani kama kwa bahati mbaya ama ajali ya kibailojia.

Chukua Muda wako Kujitathmini juu ya maisha yako ya kila siku namna unayoongea na watu,unavyowatendea watu,unavyojitendea wewe mwenyewe,kazi ,mahusiano,uchumi,biashara .

Je? Umefika unapotaka kufika? ,njia unazopita zitakufikisha pale unapotaka kufika? Uongeze nini ?,upunguze nini? Ubunifu wa aina gani unahitajika kuboresha huduma yako,kazi yako na maisha yako kwa ujumla.

Pata muda wa kuwasamehe waliokukosea na kujisamehe pia pale ulipojikosea ,Kwasababu ili kuishi maisha yenye furaha sharti moja wapo la kuzingatia ni kusamehe kila kukicha.

Kusamehe ni muhimu kwasababu katika mikiki mikiki ya maisha kuna mikwaruzano ,kukanyagana ili mradi kuyafikia maisha yako.

Chukua muda wako kuwashukuru wale wote ambao wamekua wema kwako kwa namna moja au nyingine na kuchangia kukufikisha hapo ulipo ,shukuru hata kwa machache utakirimiwa mengi.

Tumia muda wako wa ziada kuboresha kazi yako,biashara yako,kipaji chako ili kuleta manufaa tarajiwa.

Jifunze mbinu mpya za mapambano nje ya uwanja wa mapambano ili ukiingia kwenye uwanja wa mapambano uweze kushinda .
Ibua ubunifu mpya na utofauti utakaokuwezesha kuliteka soko  acha kufanya mambo ya kawaida kila siku yanayofanya maisha yako kuwa ya kawaida,biashara ya kawaida,uchumi wa kawaida,Kataa kuwa wa wakawaida,kuwa Mbunifu kuwa wa Tofauti.

Tumia muda wako wa ziada kujifua mithili ya mwanajeshi anayejua mbele yake kuna vita ya maisha na anahitajika kupambana na kushinda .

Tumia   muda  wako  wa  ziada  kutengeneza  ushindi  wa  kesho  hata  kama  leo  ulishindwa.

Maisha ni kama mchezo leo unaweza kushindwa kesho ukashinda usikate tamaa jiandae kushinda.

Tumia muda wako kwa nidhamu ,tumia fedha zako kwa nidhamu,tumia nguvu zako kwa nidhamu,tumia akili zako kwa nidhamu.

Nakutakia Ushindi na Mafanikio katika Kila jambo jema la kimaendeleo

0765938008




About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top