PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: ONA Uteuzi mwingine alioufanya Rais Magufuli leo August 25 2016
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Leo August 25 2016 Rais wa Jamhuri ...


Leo August 25 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).

Andrew Wilson Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Uteuzi wa Bw. Andrew Wilson Massawe unaanza mara moja.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top