Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza katika
hafla ya kukabidhi hundi ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya mji wa
Kahama, hafla hiyo ilifanyika baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi
madarasa ya shule ya
msingi Budushi na nyumba za walimu Mwime.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakishuhudia wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi
Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akihutubia wananchi wa
Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma yenye thamani ya
zaidi ya shilingi milioni 700
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu wakati wa makabidhiano ya hundi ya malipo ya huduma.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma
Na Dixo Busagaga
Mgodi
wa Buzwagi umekabidhi wa halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba na kumi na saba
(717,276,055/=) ikiwa ni sehemu ya malipo
ya kodi ya huduma(service levy) ambayo hulipwa kwa halmashauri hiyo.
Akizungumzia
malipo hayo ya hundi Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa
Mwaipopo amesema kiasi hicho ni malipo ya kuanzia mwezi januari hadi
juni mwaka huu.
Mwaipopo
ameongeza kuwa licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali na
kujishughulisha katika kufadhili miradi ya Maendeleo, amesema ipo haja
ya Jamii kuilinda na kuitunza miradi hiyo ili iwe na
manufaa kwa Jamii nzima.
“Acacia
kupitia Mgodi wetu wa Buzwagi tunajivunia kuwa wadau muhimu wa
maendeleo wa halmashauli ya mji wa Kahama na serikali kwa ujumla, na
tunafarijika sana kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata,
ombi letu kwa Jamii zinazonufaika na miradi yetu kuilinda na kuitunza kwa manufaa ya Jamii nzima.”
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea hundi ya kodi ya huduma kutoka kwa uongozi wa
Mgodi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri
ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo
wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika
kutekeleza miradi ya Maendeleo”
Akizungumza
kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri
hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea
kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.
Post a Comment