PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: DIGREE /DIPLOMA SIYO KAZI SEHEMU YA III
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA ADSON KAGIYE Zamani kidogo walisema -kazi ni utu, kazi ni uhai- hawakukosea. Bila kazi huwezi kula, kuvaa na kulala pa zuri....

https://lh6.googleusercontent.com/-xIpjgqv2UcA/AAAAAAAAAAI/AAAAAAAAAAA/F_1A0MyWG1s/s128-c-k/photo.jpg
NA ADSON KAGIYE

Zamani kidogo walisema -kazi ni utu, kazi ni uhai- hawakukosea.
Bila kazi huwezi kula, kuvaa na kulala pa zuri.
KAZI BASI ni shughuli yeyote inayompatia mtu mahitaji muhimu au tuseme ya lazima.
Kazi si ajira
Kazi si Elimu
Kazi si uzoefu
Kazi sio pesa.
Kazi ni kazi yaani shughughuli (activity) yeyote ukupatiayo mahitaji muhumi, inaweza kuwa pesa, chakula, Nguo au mahala pa kulala.
Maana yake ni kwamba unaweza kuwa na ajira ambayo si kazi kwa kuwa haikidhi mahitaji yako muhimu, yaani wewe unafanya kazi ambayo haiwezi kukulisha, kukuvalisha na kukupa hifadhi yako.
Pia unaweza kuwa na ujuzi flani, lakini ujuzi huo bado haujakuletei mahitaji muhimu yanayotakiwa.
Nyere akasema Uhuru na Kazi. Mimi nasema Elimu na Kazi.
Hii inakuwa ngumu kumeza kwa kuwa kuna watu hawana degree na wanakazi, na kuna wengine wana degree na hawana kazi. Tofauti IPO wapi?
Ujuzi na Elimu uliyonayo mtu lazima uende katika hali halisi ya maisha na kuanza kutatua matatizo ya jamii na kisha jamii kukulipa, au elimu uliyonayo inatakiwa itumike kuunda mifumo mbalimbali ya kubadilisha Mali asili au malighali na kuwa Mali mazao.
Mkulima hutumia ujuzi wake na elimu Yake ya kurithi ktk kilimo na kubadili malighali ya nguvu zake, ardhi, muda na mbegu na kuwa chakula. Hapo anakuwa amefanya kazi na kuzalisha mahindi.
Sasa ishu kubwa inayobakia ni kuwa kwa nini basi huyu Mwenye degree/diploma hawezi kubadili malighafi zinazomzunguka na kupata Mali mazao na kisha kukidhi mahitaji yake?
Tumeona fursa Zipo, pingamizi ni nini.?
Endekea kushiriki nasi ktk mjadala huu kwa kuchagua jibu mojawapo ya Haya hapa chini
Kama umeona fursa pingamizi ni nini?
Au tuseme kwa wale walio ona fursa unadhani pingamizi zao ni zipi?
A. Uoga na wasiwasi
B. Mtaji
C. Ukosefu wa mitandao imara ya kifedha na masoko
D. Ukosefu wa ujuzi na uzoefu
E. Andika yeyote unayofikiria
Na Adson Kagiye
 
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top