PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Degree /Diploma sio kazi sehemu ya sita
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Kuna vitu according to me lazima uwe navyo na kuna vitu ni optional. Mfano 1. Connection ni lazima 2. Ujuzi wa kuuza na k...


Kuna vitu according to me lazima uwe navyo na kuna vitu ni optional. Mfano
1. Connection ni lazima
2. Ujuzi wa kuuza na kujiuza n lazima.
3. IT and computer application a must
Kuna siku mtu nimemwombea kazi mahali akaitwa interview, what happened akakosa kazi.
Yaani connection alikuwa nayo ambayo ni Mimi lakini hakuweza kujiuza. Nilipomwuliza jamaa wa interview akaniambia mtu wako ni average person hakuweza kuvuka pass mark yetu ya 50%.
Unaweza kuwa na uwezo wa kutengeneza logo
Kwa mfano, lakini usiweze kuuza hizo logo zako simply because huwezi kuzifanyia marketing, unaweza kuwa umeandika kitabu chako kizuri sana lakini huwezi kiuza. Safari moja nilikuwa na Asali drum5 kama tani 1 hivi zilikaa ndani kwa miezi mi4. Hata baada ya kutangaza sana hazikutoka. Nilipobadili gia nakuanza kuelezea malkia wa nyuki na vitu vingi vya tofauti kuhusu nyuki kama 'bees morning meeting' oda zilianza kuja kwa fujo as far as Zambia.
Lazima ujifunze kusoma mind za watu. Hata ukienda interview jaribu kuwasoma wanaokusaili kwa haraka, jifunze wanajua nini na hawajui nini. Interview yangu ya mwisho ambayo ilikuwa na interviewer 12 swali moja la kijinga  waliniuliza ni kuwa kama usingekuwa mhasibu ungekuwa nani nikawambia ningekuwa mpishi it was like  why nikawambia mimi napenda sana kula na kulisha watu chakula bora si bora chakula. Tulivotoka nje Bonge moja akanifuata immediately kuongea naye kidogo tu nikamuuzia menu zangu za kupunguza uzito kwa bei ya juu sana.
Every opportunity has a good side effect
Kuwa muuzaji jiuze na uza bidhaa, connection ndio utapata lakini je unaweza jiuza, unaweza uza bidhaa yako kwa kutumia mbinu za tofauti.
Ingia YouTube, facebook, ukiona coz za sales usikose kuzusoma,  usiseme hizo ni coz za marketing me daktari hazinihusu au mi mwanasheria hazinihusu.
So long as you will be selling something even your own degree/labor, learn to be a sales person
PAMOJA NA networking au connections au mitandao au mifumo, kuna ujuzi wa kuuza na ujuzi wa kompyuta, pia kuna ujuzi wa kusoma na kuandika na ujuzi wa mawasiliano na mwisho ni ujuzi wa namba na ujuzi wa saikolojia.
Sasa wengi wenu mnakimbia namba, English hamjui, kiswahili hamjui je uwezo wa kuuza utautoa wapi?
Inapoandikwa kwenye gazeti asilimia 40 ya watanzania wanakisukari na gazeti lingine linaandika asilimia 49 ya wanandoa ni wachepukaji..
How do you define these numbers, umesoma ndio inachekesha au kufurahusha lakini je kuna fursa hapo?
Unaposoma sensa kwamba asilimia 70 ya watanzania ni vijana na watoto chini ya miaka 21, unaelewa na unajua maana ni nini baada ya miaka 10?
Nambaz don't lie, kwenye izo namba chunguza opportunity. Kuwa na uwezo wa kuzichakata namba kubwakubwa (bulk mathematics) ndio utaweza kuwa salesman Mkubwa.
Unaweza kuwa na ndoto kubwa inayohitaji umiliki wa kampuni, kama huwezi uza wazo lako mbele ya wenye mitaji, kama hutaweza kucheza na namba wazo lako litafilia mbali kabisa.
Nambaz ni  topic hasahasa masuala ya supply and demand, mambo ya statistics, mambo ya sensa na elimu ya fedha
Ukiwa Chuo vitu hizi zote zipo free of charge, usidharau ukisikia Leo kuna semina ya communication skills, usidharau usikiapo Leo kuna semina ya namba aka statistics, tafuta muda hudhuria. Kama hazipo soma mwenyewe na uliza maswali kwa wanaojua.
Singependa sana kuongelea connection na kompyuta mana hilo liko wazi sana.
 
Imeandikwa na Adson Kagiye

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top