Msanii wa Sanaa ya Sarakasi akiendesha baiskeli ya tairi moja katika tamasha la wasanii wa filamu (TDFA) lilifanyika jijini Arusha jana katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.Picha na Ferdinand Shayo |
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wasanii wa
Filamu nchini kote wametakiwa kutumia mandhari za asili zilizoko katika maeneo
ya hifadhi za taifa kwenye shughuli zao
za kurekodi filamu badala ya kutumia majengo ya kifahari ili kutangaza utalii
kwa kupitia kazi zao.
Hayo
yameelezwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika
la Hifadhi za Taifa TANAPA ,Pascal Shelutete wakati akizungumza katika Tamasha
la Chama Wasanii wa filamu jijini Arusha
(TDFA) lililofanyika katika viwanja vya
Sheikh Amri Abeid .
Shelutete
amesema kuwa Tanapa itatoa ushirikiano kwa wasanii watakaoonyesha nia ya
kurekodi filamu zao katika maeneo ya hifadhi ambayo ni salama nay a kuvutia
yenye maparomoko ya maji na mandhari za kuvutia ambazo zitasaidia kuhamasisha
utalii ambao kwa sasa unaongoza kuchangia pato la taifa.
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii hao
Fredrick Kefas amewataka wasanii kutumia taaluma yao katika kuhimiza utalii wa
ndani utakaoliingizia taifa pato kubwa na kuinua uchumi wan chi hivyo
kuondokana na utegemezi.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini
(TAFF) Simon Mwakifamba amewataka Wasanii kutumia vizuri fursa ya maonyesho ya
kimataifa ya filamu yanayojulikana kama
Tanzanite International Film
Festival yatakayojumuisha wasanii mahiri wa filamu kutoka nchi mbalimbali
duniani ikiwemo Marekani,Asia ,Australia .
Alisema Tamasha la Wasanii wa Filamu jijini Arusha lilipambwa na michezo
mbali mbali ikiwemo timu ya mpira wa miguu ya wasanii wa Kilimanjaro na Wasanii
wa Arusha,timu za mpira wa miguu za mkoani Arusha pamoja na mchezo wa netiboli,Michuano bado
inaendelea ambapo mshindi wa kwanza atapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya
Manyara na Ngorongoro.
Post a Comment