Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wabunge wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Viwanda na
Biashara wamemtaka Rais John Pombe Magufuli kulitumbua jipu shirika la umeme
Tanesco kwa kununua transfoma kutoka nje ya nchi licha ya kumiliki asilimia 20%
ya hisa katika kiwanda cha Tansfoma cha Tanalec kilichopo jijini Arusha .
Kamati hiyo
ya Bunge imebaini hayo jana wakati wa ziara yao ya kutembelea viwanda jijini Arusha
ili kufahamu changamoto na kasi ya ukuaji wa viwanda ambapo Wabunge hao
wameshangazwa na kitendo cha Tanesco kutonunua transfoma katika kiwanda hicho
ambazo huuzwa katika nchi jirani za Kenya ,Zambia Malawi na Burundi.
Mbunge wa
Arusha mjini Godbless Lema ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo alisema kuwa ni
jambo la kushangaza kwa Tanesco ambao ni wamiliki wa Tanalec na wako katika
wakurugenzi wa bodi lakini bado wanaagiza transfoma nje ya nchi suala ambalo
linapaswa kutazamwa kwa umakini na kupatiwa majibu.
“Tunashindwa
kuilewa Tanesco kwanini wanafanya hivyo wakati kiwanda ni cha kwao na wakati Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba yuko ndani ya bodi ya wakurugenzi ,hapa kuna
mgogoro ambao unapaswa kuatatuliwa kwa wakati ili kunusuru kiwanda hiki”
Alisema Lema
Naye Mbunge
wa Singida Mjini Musa Sima wamesema kuwa uamuzi huo wa Tanesco kununua transfoma za nje ya nchi unazorotesha ukuaji
wa viwanda vya ndani na kukiuka adhma ya Rais Magufuli ya kujenga uchumi wa
viwanda nchini kwani ni vigumu
kukuza viwanda wakati bila kuvilinda viwanda vya ndani dhidi ya bidhaa za nje.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Vicky Kamata
na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dalali Kafumu wameitaka serikali kuchukua
maamuzi juu ya suala hilo la Tanesco ili kulinda viwanda vya ndani viweze
kuchochea maendeleo ya Taifa.
Meneja Mkuu wa Tanaleck Zahir Salehe ameiomba serikali
irekebishe sheria za manunuzi ili zitoe kipaumbele kwa viwanda vya ndani viweze
kukua na kutoa ajira nyingi hivyo kukuza pato la nchi.
Post a Comment