Na
Ferdinand Shayo,Arusha.
Vituo vingi
vya polisi hasa vile vilivyopo pembezoni mwa miji vimekua vikikabiliwa na
changamoto ya uchakavu wa majengo,uhaba wa majengo pamoja na vitendea kazi
suala ambalo linapunguza kasi ya jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu.
Hayo
yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha aliyemaliza muda wake Liberatus
Sabas amesema kuwa uhaba wa majengo na vituo katika maeneo ya vijiji umekua
ukipunguza ufanisi wa kazi ya polisi katika kulinda raia na mali zao hivyo
ameitaka serikali kukarabati vituo hivyo pamoja na kuweka vitendea kazi vya
kutosha.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kituo kipya cha polisi cha Tengeru kilichozinduliwa rasmi na
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa hatua ya kuboresha
vituo vya polisi itasaidia kutatua kero za kiusalama zinazokabili maeneo mengi
mkoani Arusha.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Meru amelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua baadhi ya
polisi ambao huwabambikia wananchi na kujihusisha na vitendo vya rushwa ambavyo
huwaumiza wananchi wengi
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha aliyezindua kituo hicho amewataka Wananchi wa kushirikiana vyema na
jeshi la polisi katika kutoa taarifa za uhalifu ili kutokomeza vitendo vya
uhalifu vinavyojitokeza kila mara
|
Post a Comment