Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete Rais mstaafu wa Tanzania kwa awamu ya nne (2005 –
2015) ni miongoni mwa wanadiplomasia wakubwa duniani wenye ushawishi na
uwezo wa utatuzi wa matatizo mbalimbali duniani, sio tu kwa sababu
viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanamkubali bali kwa uwezo wake
katika masuala ya kidiplomasia.
Alizaliwa
mwaka 1950 Oct katika mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo katika kijiji
cha Msoga katika familia ya kisiasa na kilimo. Baba yake Mzee Mrisho
Kikwete alikuwa ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Pangani na babu yake naye
ambaye alikuwa ni Chief wa Wakwere, Chief Kikwete.
Alipata
elimu ya Msingi Msoga kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Kibaha
akiwa pia ni mwenyekiti serikali ya wanafunzi na vijana wa TANU 1966 na
Baadaye Tanga school. Ambapo alijiunga na chuo kikuu Dar es salaam,
ambapo pia alikuwa mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi na kuhitimu
Shahada ya uchumi 1975 alipojiunga na Jeshi.
Aliteuliwa
kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Singida 1977 na baadae
kuhamishiwa Zanzibar kwa kazi maalum baada ya muungano wa TANU na ASP
mpaka kufikia mwaka 1980 aliporudishwa makao makuu ya chama (CCM).
Mwaka
1988 aliteuliwa kuwa mbunge na pia NaibuWaziri wa Nishati na Madini
chini ya uongozi wa MH. Al Ahsan Mwinyi mpaka kufikia mwaka 1990 ambapo
aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa maji nishati na madini.
Mwaka
1994 aliteuliwa kuwa waziri wa uchumi akiwa na umri wa miaka 44 ambapo
alikuwa ni waziri mwenye umri mdogo kuwahi kuteuliwa. Kufika mwaka 1995
alitueliwa kuwa waziri wa mambo ya nje chini ya uongozi wa Rais Benjamin
W. Mkapa na kuongoza wizara hiyo kwa miaka 10 mpaka kufikia mwaka 2005
ambapo alichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.
Katika
Nyanja za kimataifa Mh. Jakaya Kikwete ni miongoni mwa wanadiplomasia
ambae amefanya mambo mengi katika bara la Afrika na Dunia, kama vile
kutatua migogoro katika nchi za maziwa makuu, jumuiya ya Afrika
Mashariki akiwa kama Mwenyekiti wake (EAC) baadhi ya mambo ambayo dunia
inampongeza ni pamoja na Mwaka 2005 akiwa kama Mwenyekiti mwenza wa
mikutano wa Helsinki (Helisinki process on Globalization and Democracy)
aliweza kuongoza mikutano huo kwa mafanikio makubwa.
2013
akiwa ndiye kiongozi pekee kutoka Afrika aliyeshiriki katika mkutano
nchi za umoja wa Ulaya EU wa Alpbach Austria aliliwakilisha bara la
Afrika vyema katika kutafuta fursa za maendeleo na ushirikiano
kimataifa.
Dr.
Jakaya Kikwete pia amekuwa Mjumbe tume ya Elimu Duniani ikiongozwa na
waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown katika kutafuta namna ya
kugharamia Elimu duniani (TICFGEO) kwa mwaka 2015.
Kwa
mwaka huu 2016 Dr. Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa Mjumbe wa kamati ya
Amani nchini Libya katika kusaidia kurudisha amani nchini Libya
Pia
amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mwenza kwa tume ya kusaidia afya ya Mama
na motto duniani kwa mwaka huu 2016 ikiwa ni katika jitihada zake
kuhakikisha Afya na mama na motto duniani kote zinalindwa.
Kwa
mtazamo huo nina imani kubwa kwa kipindi ambacho Mh. Ban Ki-Moon
ataachia ofisi, Mwanadiplomasia huyu ndiye atakayechukua viatu vyake .
Hizi ni baadhi ya tuzo za heshima alizowahi kupata toka nchi mbalimbali...
2007: Sullivan Honor
2007: The AAI African National Achievement Award (on behalf of Tanzania).
2009: US Doctors for Africa Award.
2011: Social Good Award from the United Nations Foundation
2011: South-South Award for Global Health, Technology and Development
2012: FANRPAN Policy Leadership Award from the Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network.
2013: Africa's Most Impactful Leader of the Year by the Africa Leadership Magazine
2013: ICCF Mengha Award by the International Conservation Caucus Foundation
2014: Icon of Democracy Award, from The Voice Magazine (Netherlands)
2015: Leadership Excellence Award by the Pan-African Youth Union.
2015: African Achievers Award by the Institute for Good Governance in Africa.
2015: African Statesman of the Year by the The African Sun Times.
Post a Comment