Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Njia
mojawapo ya kushinda ni kuondoa mawazo ya kushindwa kwenye kila jambo la
kimafanikio unalotaka kufanya.
Watu wengi
wanashindwa kufanikisha maisha yao ya kiuchumi ,kijamii na kibiashara kwasababu
ya kutawaliwa na mawazo ya kushindwa yamekua mengi kuliko mawazo ya kushinda
katika akili na mawazo yao.
Hili ni
Tatizo kubwa duniani ambalo limekua
likizuia mafanikio ya watu wengi na kufanya ndoto nyingi zife.
Mawazo ya
kushindwa na mtazamo hasi ni kama bomu ambalo linasambaratisha mawazo mazuri
aliyoyanayo mtu,ndoto na maono.
Kumbuka kuwa
wazo zuri moja ulilonalo ukilifanyia kazi linaweza kukupa mafanikio makubwa na
maisha mazuri unayoyataka.
Fikiri juu
ya mawazo mabaya uliyonayo yanakupa nini katika maisha yako sana sana yanakupa
kushindwa katika mambo mengi ya
kimafanikio unayojaribu kuyafanya.
Inatupasa
kuwekeza kwenye kuwaza vizuri,kufikiri vizuri ili tuweze kutenda vizuri na
kufanikisha mambo yetu.
Mtu mmoja
aliwahi kusema kuwa mtu ni matokeo ya mawazo yake maana yake jinsi unavyowaza
ndivyo utakavyokua ,jiulize unawaza nini?
“Mawazo mazuri yanaweza kutengeneza
maisha yako na mawazo mabaya yanaweza kuyaharibu maisha yako”
Kumbuka kila
kitu unachokiona duniani kilikua ni mawazo ya watu na ndoto zao kama vile
kompyuta,simu,gari,mavazi, majengo makubwa kwa madogo na vitu vingine vingi.
Jiulize kuwa
una mawazo gani ambayo yanaweza kukufikisha kwenye mafanikio unayoyataka na kukupa maisha unayoyataka.
Yatupasa
kuwekeza kwenye mawazo yetu na fikra zetu ,kutengeneza mitazamo chanya
itakayokufikisha kwenye mafanikio.
Mtazamo ni kama msingi wa nyumba ,ukiwa na msingi
mbovu nyumba haiwezi kusimama hata kama inapakwa rangi nzuri kiasi gani lazima itaanguka tu na kwa
binadamu ni hivyo hivyo.
Uwe na
uhakika kuwa ukiwa na mtazamo hasi utaanguka tu haijalishi unavaa suti ,una
pesa kiasi gani kwa sababu mtazamo ni msingi.
Ukitaka
kutengeneza mtazamo chanya inakupasa inakupasa kuepuka kukaa na watu wenye
mtazamo hasi watu ambao wamejaa mawazo ya kushindwa .
Watu ambao
ukiwaambia jambo wanakukatisha tamaa watu ambao wameshindwa kabla hata
hawajaanza kutokana na mtazamo wao hasi.
Kaa mbali na
watu kama hao ukitaka kufanikiwa maana “Ukitaka kupaa kama Ndege aina ya tai
tafuta marafiki ambao wanapaa kama tai usikae na marafiki wanaoiashi
kama kuku kupaa kwako itakua ndoto utabaki kuishi maisha ya chini.
Tazama
vipindi vya runinga,redio na magazeti ambayo yanakupa hamasa na ari ya kutimiza
ndoto zako vitu ambavyo vinakujenga
zaidi na si kukuharibu .
Usijaze
habari za mauaji,ukatili kwenye kichwa chako jaza vitu ambavyo vitakupa afya za
kusonga mbele na kutimiza ndoto zako.
“We became
what we think” maana yake Tunakua vile tunavofikiria .Ni vyema kujizuilia kufikiria vibaya juu yako na
kuwafikiria vibaya wengine ili kutengeneza mtazamo chanya.
Jitaidi sana
ukionyeshwa donate usione tundu uone donati
na huo ndo mtazamo chanya hata
katika giza unaweza kuona mwanga kutokana na mtazamo wako na katika matatizo
unaweza kuona suluhu kutokana na mtazamo wako.
Mtu mmoja
aliwahi kusema kuwa akili yako ni kama
benki utakachokiingiza ndicho utakachokitoa
akionyesha umuhimu wa kuwa makini na vitu tunavyoviingiza vichwani
mwetu.
“Your Mind
is like a Bank what you Deposit is what you Withdraw”
Kuwa makini
na kila unachokiingiza kichwani kwako,Nakutakia mafanikio kwenye maisha yako
0765938008
Post a Comment