PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Mapumziko ya Rais Magufuli Nyumbani Kwake Geita Yawapasua Vichwa Viongozi
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mapumziko ya Rais John Magufuli nyumbani kwao, Chato mkoa wa Geita, yanaonekana kuwapasua vichwa viongozi wa serikali ya m...


Mapumziko ya Rais John Magufuli nyumbani kwao, Chato mkoa wa Geita, yanaonekana kuwapasua vichwa viongozi wa serikali ya mkoa huo kutokana na kutoelewa ratiba yake kwa muda atakaokuwapo nyumbani hapo.
Rais Magufuli aliwasili juzi mjini Chato akitumia usafiri wa helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyotanguliwa na helikopta ya polisi, kabla ya kuwahutubia wananchi wa wilaya hiyo.
Ujio huo ni wa kwanza tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Oktoba 25, mwaka jana.
Hata hivyo, Nipashe jana ililazimika kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe, ili kufahamu ratiba ya shughuli atakazofanya Rais Magufuli muda atakaokuwapo hapo.
Hata hivyo, hali hiyo imeonekana pasua kichwa kwa viongozi hao, baada ya mkuu wa wilaya kudai tangu Rais awasili nyumbani kwake, viongozi hao walielekezwa kuendelea na majukumu yao ya kawaida. 
"Ukweli viongozi hatuna ratiba yoyote zaidi ya mapumziko, maana tangu amewasili nyumbani tulielezwa kuendelea na kazi zetu za kawaida na Rais atakapotaka kufanya jambo atatujulisha kupitia kwa mkuu wa mkoa,” alisema Ntarambe.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli juzi aliwapongeza wananchi wa Chato kwa kujitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wake wa hadhara, licha ya kuchelewa kutoa taarifa za ujio wake kwa kuwa hakupenda kupokewa kwa kishindo kwa sababu huko ni nyumbani kwao.
Nawapongeza kwa kunipokea. Najua wengi mmepata taarifa za ujio wangu kuanzia jana (juzi) saa 11. sikupenda kupokewa maana nakuja nyumbani, ndiyo maana kila napogeuka hapa nawaona wazee wangu mpo hapa wengi," alisema.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top